Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, October 25, 2016

WAZEE LUDEWA WAANZA KUNUFAKA NA MATIBABU BURE




NJOMBE

Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Imeanza Zoezi la kuwashawishi wazee wote waliofikisha umri wa miaka 60 na kuendelea kuchukua vitamburisho vya kupatiwa matibabu bure ili kuwasaidia kutibiwa katika zahanati,vituo vya afya na Hospitali.

Akizungumza  Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema wazee wenye umri wa miaka kuanzia sitini na kuendelea Wilayani humo wanapaswa kupatiwa huduma za matibabu bure kama ambavyo miongozo ya sera ya wizara ya afya inavyosema na kutaka  halmashauri kuwaandalia vitamburisho ili waepukane na usumbufu kwenye vituo hivyo.

Aidha bwana Tsere ametaka wananchi ambao hawajajiunga na mfuko wa Taifa wa afya CHF Kuchangia kiasi cha fedha shilingi elfu kwaajili ya kupata matibabu kwa familia nzima mwaka mzima pasipo kupata usumbufu wowote wa kulipia huduma za matibabu waendapo sehemu za afya.

Amesema serikali za vijiji na kata zinatakiwa kuwatambua wazee waliopo kwenye maeneo yao na kuwaweka kwenye orodha ya kupata huduma za matibabu bure ambapo orodha hizo zinapaswa ziwepo hata kwenye ofisi zao baada ya kuwatambua huku zahanati na vituo vya afya navyo vikitakiwa kuondoa usumbufu kwa wazee wanaofika kupatiwa matibabu.

Kwa upande wao wazee waliopo Wilayani Humo wamepongeza kwa hatua inayoendelea kufanywa na serikali ya kuyakumbuka makundi ya wazee kwani tayari baadhi yao wameanza kupata huduma za matibabu bure huku wengine wakisema bado kuna tatizo la kukosekana kwa dawa pindi wanapokwenda kutibiwa kwenye zahanati zilizopo karibu nao.

No comments:

Post a Comment