Sunday, September 25, 2016
WAZEE KATA YA MAKOGA WALIA NA PENSHEN NA VITAMBURISHO VYA MATIBABU BURE
WA UPANDE WA KULIA NI MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA NG'ANDA NA WA KATIKATI NI DIWANI ALIYEKUWEPO KWA NIABA YA MBUNGE WA JIMBO LA WANGING'OMBE Danroad Mgaya NA WA TATU NI MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE KATA YA MAKOGA Lutengano Mgaya
Lutengano Mgaya MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE MAKOGA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KWENYE SHEREHE ZA WAZEE
WAZEE MBALIMBALI WA KUTOKA VIJIJI SABA VYA KATA YA MAKOGA WAKIWA KWENYE SHEREHE ZA WAZEE ILIYOFANYIKIA KIJIJI CHA NG'ANDA
BURUDANI YA NGOMA NAYO IKACHUKUA NAFASI YAKE
Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya wanaohusika na matukio ya mauaji kwa wazee ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo ambao wanapatikana katika vijiji mbalimbali Mkoani Njombe.
Rai hiyo imetolewa na wazee wa kata ya makoga wakiwa kwenye sherehe yao iliyofanyikia katika kijiji cha Ng’anda Wilayani Wanging’ombe ambapo wametoa kilio hicho kwa serikali ili iwatatuliye ikiwemo kupewa huduma za matibabu bure.
Aidha wazee hao kupitia risala iliyosomwa na afisa mtendaji Alberto mpwaga wameshukuru shirika la PADI Ambalo limekuwa likiwapatia mikopo midogo kwaajili ya kuendesha shughuli za miradi ya ufugaji kuku,nguruwe na kilimo cha bustani huku akibainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni kukosa mfuko wa kujiendeleza.
Akizungumza na baadhi ya wazee wa kata ya makoga kwa niaba ya mbunge wa jimbo hilo diwani wa kata ya makoga Danroad Mgaya ameomba kila kijiji kifanye kazi ya kufungua akaunti za benki na kuahidi kuzifikisha sehemu husika changamoto zilizowasilishwa na wazee kwenye sherehe hizo.
Awali Mwenyekiti wa baraza la wazee kata ya Makoga Lutengano Mgaya ameshukuru uongozi wa kata ya makoga kwa kuonesha ushirikiano kwa kundi la wazee waliopo kwenye kata hiyo na kusema baraza la wazee kata ya makoga linahamasisha vijana kuzingatia maadili ili kutunza utamaduni wa kila jamii.
Kwa upande wao baadhi ya wazee wameomba kuboreshewa huduma za matibabu katika maeneo yao kwa kuwatengenezea vitamburisho vitakavyowaruhusu kupatiwa huduma za matibabu popote watakapo kwenda huku wakishukuru kwa jitihada zilizofanywa hadi sasa kwani baadhi yao wanapata huduma za matibabu bure.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment