Mafundi
wa Shirika la Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara),
wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda
Moshi Baa Dar es Salaam jana.
Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
Pikipiki ikivushwa.
Waendesha
bodaboda wakivusha pikipiki zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda
barabara katika makutano ya Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi
Baa Dar es Salaam jana wakati mafundi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na
Zambia (Tazara), wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi
wa Shirika la Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara),
wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda
Moshi Baa Dar es Salaam.
…………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA
ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa
kutozingatia muda muafaka wa kufanyia ukarabati wa reli zake jambo
linalowaletea usumbufu.
Malalamiko
hayo waliyatoa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mwandishi wa
habari hizi kuhusu kadhia waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara
ya Mombasa kwenda Moshi Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana
na barabara hiyo.
“Kazi
ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri lakini wangekuwa wakiifanya nyakati
za usiku ili kuepusha usumbufu huu tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu
relini” alisema Gedion Robert.
Robert
alisema katika nchi za wenzetu kazi za kusafisha miji na ukarabati wa
namna hii hufanyika usiku ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia
barabara kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Mkazi
mwingine kwa Diwani Stellah Urio alisema amelazimika kulipa sh. 400
kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo pia alilipa sh. 400 baada ya
kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa na kujikuta akitumia sh.800
badala ya 400.
Jitihada
za kumpata msemaji wa Tazara , Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala
hilo zilishindika baada ya kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi
arudi baadae alikuwa nje ya ofisi kikazi.
No comments:
Post a Comment