Monday, September 19, 2016
WANGING'OMBE KUFUFUA VYANZO VYA MAPATO
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ALLY KASSINGE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ally Kassinge amewataka watalaamu wa halmashauri hiyo kufufua vyanzo vya mapato vilivyopo kwa kushirikiana na wananchi ili kuongeza mapato ya halmashauri hiyo.
Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati akiwa katika kijiji cha Igima ambapo ameagiza watalaamu wa Uvuvi kutembelea bwawa la Lihogosa na kuweka mipango ya kupandikiza samaki wengine kwaajili ya kukuza uchumi.
Kassinge ametoa Kauli hiyo kufuatia wananchi wa kijiji cha Igima kumuomba asimamia zoezi la kupandikiza samaki wengine aina ya kambale na kuhimiza uhifadhi wa vyanzo vya maji ili kurudisha hadhi ya bwawa hilo kama ilivyokuwa hapo awali.
Amesema ndani ya siku saba mtalaamu wa uvuvi Wilaya ya Wanging'ombe ahakikishe amefika katika kata ya Igima kutembelea bwawa la Lihogosa akishilikiana na viongozi wa kata ya Igima ili kuweka mikakati ya kuanzisha ufugaji wa samaki na kurudisha hadhi ya Samaki wanaostahili kufugwa.
Awali wakizungumza kwenye mkutano huo baadhi ya wananchi wa kijiji cha Igima wamesema serikali imeshindwa kusimamia ufugaji wa samaki kwenye bwawa hilo la Lihogosa na kusababisha kuwepo kwa samaki wadogo ambao wanavuliwa na kila mmoja pasipo kuwekewa utaratibu wowote.
.......................................................................................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment