Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania
waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya
Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni
Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.
Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mmiliki
wa Kampuni ya Simba Logistic ambayo magari yake na madereva walitekwa,
Azim Dewj (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva
hao.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisubiri kuchukua taarifa za kuwapokea madereva hao.
Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao.
Dereva Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
Dereva Kumbuka Seleman (kulia), akisimulia jinsi alivyotoroka na kutoa taarifa ya kutekwa kwao.
Dereva
Athuman Fadhili (kulia), akisimulia walivyookolewa na majeshi ya Congo
na jinsi walivyojificha porini na kutembea umbali mrefu kwa kutambaa
ambapo ilifika wakati waliomba bora wafe kuliko mateso waliyokuwa
wakipata.
Hapa ni furaha ya kukutana na ndugu jamaa na wafanyakazi wenzao.
Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.
Ndugu, Jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao wakiwa nje ya jengo la VIP uwanjani hapo wakisubiri kuwapokea.
Mapokezi yakiendelea.
Ni furaha ya kukutana na wapendwa wao.
Hapa Dereva Mbwana Said akikumbatia na mjomba wake Kassim Salim katika hafla hiyo kwa Mbwana ilikuwa ni furaha na majonzi.
Mbwana Said (katikati), aamini macho yake baada ya kukutana na mke wake Mariam pamoja na mtoto wake Kauzari.
…………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MADEREVA
10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya
Demokraia ya Congo (DRC) wamesema waliponea tundu la sindano kuuawa.
Kauli
hiyo imetolewa na madereva hao katika hafla ya kuwapokelewa
iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar
es Salaam leo jioni.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake Mbwana Said alisema analishukuru jeshi la Congo
kwa jitihada kubwa walioifanya kwa ajili ya kuokoa maisha yao.”
”
Tunaishukuru serikali ya Congo kwa kutuokoa kwani tulikuwa katika
wakati mgumu na leo kuungana tena na ndugu zetu” alisema Said.
Alisema
walilazimia kutembea kwa muda mrefu huku risasi zikirindima kati ya
majeshi ya serikali na waasi hao hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka
kwenye mikono ya waasi hao.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Suzan Kolimba aliishukuru serikali ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na
kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.
Balozi
wa Congo nchini Jean Mutamba aliwataka madereva hao kuacha viza na
nyaraka zao ubalozini pindi wanapo safiri na kurudi ili iwe rahisi
kuwatambua pale wanapopata matatizo.
“Tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya na kutoa wito kuwa waendelee kusafiri kwa kufuata taratibu zilizopo,” alisema Mutamba.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment