Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, September 22, 2016

Bodi ya Vyombo vya Habari vya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) yajiuzulu









Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji
wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Peoples’ Media
Communication Limited (PMCL) inayoendesha kituo cha redio Uhuru
imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj Adam O. Kimbisa.



Mwenyekiti  wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli amepokea barua ya
kujiuzulu kwa bodi hiyo leo tarehe 22 Septemba 2016 ambayo nakala yake
imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana. Barua hiyo
inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua
kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.


Bodi ya Uhuru Media Group ndiyo iliyokuwa na majukumu ya kusimamia,
kuzielekeza na kuzishauri Menejimenti ya Makampuni hayo na kubuni mbinu
na mikakati ya kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa vyombo vya habari
vya Chama.



Imetolewa na:-


CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)

MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Tarehe 22/09/2016.




 

No comments:

Post a Comment