Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, September 19, 2016

WANANCHI KATA IGIMA WANAKIWA KUCHANGIA MICHANGO YA UJENZI MADARASA


Diwani wa kata ya Igima Wilayani  Wanging'ombe Paulina Samata Mwinami Amewaomba wananchi wa vijiji vilivyopo kwenye kata hiyo kuonesha ushirikiano katika  zoezi la kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa .

Rai hiyo imetolewa na diwani huyo Bi.Mwinami wakati akizungumza na Uplands fm kihusiana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Igima.

Bi.Mwinami amesema kuwa viongozi wa serikali za vijiji wanatakiwa kuwa waaminifu wakati wa kukusanya michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Igima ambayo tayari elimu ilitolewa kupitia mikutano juu ya kuchangia ujenzi huo.

Amesema wananchi wanatakiwa kuweka kipa umbele katika kuboresha  sekta ya elimu kama serikali inavyosisitiza   kwa kujenga miundombinu ya shule ikiwemo vyoo na madarasa ili wanafunzi waweze kusomea kwenye mazingira mazuri na kuongeza kiwango cha ufaulu huku akiwaasa wazazi kuwaendeleza wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi.

Hivi karibuni kiwa kijiji cha Mng'elenge Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ally Kassinge aliwataka wananchi kuisaidia serikali kutatua baadhi ya changamoto zilizopo kwenye vijiji na kata zao zikiwemo za ujenzi wa madarasa pamoja na kukemea utoro unaojitokeza kwa baadhi ya shule.

No comments:

Post a Comment