Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, September 1, 2016

JUA LA PATWA KWA ASILIMIA 98 NJOMBE

 PICHA YA JUA LIKIWA LIMEPATWA BAADA YA HATUA KWA HATUA KUPITA
 PROFESSOR ECKEHARD  SCHMIKT  AMBAYE AGUDUA KUWEPO KWA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KATIKA KIJIJI CHA LITUNDU KATA YA WANGING'OMBE KWA ASILIMIA 98 KWA MWAKA 2016 WA KUTOKA UJERUMANI.
 JUA LIKIPATWA KABLA HALIJAWA DUARA


 MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIHUTUBIA WANANCHI WALIOFIKA KWENYE TUKIO LA KUPATWA KWA JUA HII LEO AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WA WILAYA AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ALLY KASSINGE MWENYE KOFIA NYEUPE NA TSHERT NYEUPE NA MWENYE KILEMBA NA MTANDIO SHINGONI NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.RUTH MSAFIRI NA ALIYESHIKA MIC NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

 MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIJARIBU KUANGALIA KUPATWA KWA JUA KUPITIA MIWANI MAALUMU  KWENYE ENEO LA TUKIO LA KIJIJI CHA LITUNDU


 VITABU NA VIPEPELRUSHI WATU MBALIMBALI WAMEPEWA KUSOMA KAMA HICHO ANACHOKISOMA MKUU WA MKOA
 HAWA NI WANANCHI WAMEPANGA MSTARI KWAAJILI YA KUPEWA VIFAA VYA KUTAZAMIA JUA LINAPOPATWA KWANI HATAKIWA MTU KUTAZAMA JUA LINAPOPATWA PASIPO KUVAA MIWANI MAALUMU.


 KATIBU WA MKUU WA MKOA DANIEL NGALUPELA NAE AKITUMIA MIWANI MAALUMU KUANGALIA JUA LINAPOPATWA
 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE ANTON MAHWATA AKIANGALIA JUA LINAPOPATWA HII LEO


Na Michael Ngilangwa-Wanging'ombe -Njombe

Mmia ya Watanzania na Mataifa ya nje ya Nchi    leo wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua lililopatwa kwa asilimia 98 na kuweka historia Mkoani Njombe na Duniani kwa ujumla.

Tukio hilo la kupatwa kwa jua limetokea katika kijiji cha Litundu kata ya Wanging’ombe ambapo Jua limepatwa kwa asilimia 98 limetoa fursa ya kujengwa mnara wa  kihistoria  na shule   ili wageni na wanafunzi wafike kujifunza.

 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada  ya kupatwa kwa jua Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi amewasisitiza wananchi kufuata masharti wanayopewa na watalaamu kuwa watumie miwani maalumu kutazama jua hilo.

Dkt Nchimbi ametumia fursa hiyo  kuwaomba wawekezaji mbalimbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi kuwekeza kwenye sekta ya utalii na viwanda Mkoani Njombe ambapo serikali ilikwisha anza maandalizi ya kuimarisha vivutio vilivyopo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Upl Safari Gabriel Shawa amesema kukamilika kwa tukio la kupatwa kwa jua katika kijiji cha Litundu kampuni hiyo imeahidi kutoa ushirikiano kwa serikali Nchini katika kuhamasisha utalii.

Bwana Shawa Amesema kijiji cha Litundu kimepewa tani tano ya mifuko ya saruji kupitia mapato yaliyopatikana kwenye tukio hilo na kuahidi kuleta mabadiliko ya Utalii katika eneo la kusini mwa  Tanzania.

Wakizungumza na Uplands fm Baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo la kupatwa kwa jua wamesema tukio hilo limewapatia fursa ya  kushirikiana na serikali kuboresha vivutio vya Utalii viliopo mkoa wa Njombe.

Tukio la Kupatwa kwa jua kwa mara ya mwisho lilipatwa mwaka 1977 ambapo kwa sasa tukio kama hilo  linasadikika kuja kutokea tena baada ya miaka takribani mia tatu hamsini katika eneo hilo la Litundu huku tukio kama hilo kila mwaka hutokea katika Nchi Nyingine.


Tukio la Kupatwa kwa jua hii leo limeanza saa nne na dakika kumi hadi saa tano na dakika hamsini na nane wakati kila mwananchi aliyekuwepo kwenye tukio akiwa na shauku ya kutaka kutazama na hivyo walianza kutafuta miwani iliko ili kushuhudia kupatwa kwa jua.

Tukio hilo limetokea kwenye kijiji cha Litundu kata ya Wanging'ombe kilichopo umbali wa kilomita 30 kutoka halmashauri ya mji wa Makambako na kuna umbali wa mita sabini kutoka barabara kuu ya Makambako-Mbeya.

...............................................................................................................................................................

No comments:

Post a Comment