Thursday, August 25, 2016
WATALAAMU WA HALMASHAURI WILAYA YA NJOMBE WATAKIWA KUTEMBELEA MAENEO YAO YA KAZI SIYO KUKAA MAOFISINI
Watalamu Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Wametakiwa Kuyatembelea Maeneo Mbalimbali Ya Utekelezaji Wa Majukumu Yao Na Siyo Kukaa Ofisini Wakisubiri Waitwe Na Madiwani Wa Kata Zilizopo Wilayani Humo Ndipo Wafike Sehemu Zao.
Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Ruth Msafiri Ameitoa Rai Hiyo Hivi Karibuni Wakati Akiongea Na Madiwani Wa Halmashauri Hiyo Kuhusiana Na Utekelezaji Wa Majukumu Ya Wataalamu Kwa Wananchi Walioko Vijijini .
B. Msafiri Amesema Ni Wajibu Wao Watalaamu Kuwatembelea Wananchi Lakini Siyo Kukaa Maofisini Wakisubili Waitwe Na Madiwani Kwenda Kutatua Changamoto Zinazowakabili Wananchi Na Kusema Hilo Ni Agizo Kwa Kila Mtumishi Kuyafikia Maeneo Ya Kazi Siyo Kuitwa Na Kila Kata Iwe Na Mtalamu Mmoja.
Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Valentino Hongori Amekili Kuwepo Kwa Tatizo La Baadhi Ya Watumishi Ambao Wanasubili Wapate Malalamiko Kutoka Kwa Viongozi Wa Vijiji Ambapo Amelazimika Kumuagiza Mkurugenzi Kusukuma Wataalamu Wayafikiye Maeneo Ya Vijijini.
Bwana Hongori Amesema Uwajibikaji Wa Watumishi Itaisaidia Halmashauri Hiyo Kufanikiwa Katika Uzarishaji Na Ukusanyaji Wa Mapato Kutoka Kwenye Vyanzo Vyake Kwa Kutoa Elimu Za Uibuaji Miradi Mipya Ya Wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment