Jeshi La Polisi Wilaya Ya Ludewa Mkoa Wa Njombe Limewataka Wananchi Wilayani Humo Kuonesha Ushirikiano Kwa Jeshi Hilo Kwa Kutoa Taarifa Za Uharifu Ambao Unafanywa Na Askali Polisi Dhidi Ya Wananchi Kinyume Na Sheria.
Rai Hiyo Imetolewa Na Kamanda Wa Polisi Wilaya Ya Ludewa Emmanuely Gariyamoshi Wakati Akizungumza Na Wananchi Wilayani Humo Na Kusema Kuwa Amepokea Malalamiko Mengi Yanayohusu Askali Wake Ambao Wamedaiwa Kufanya Kazi Kinyume Na Sheria Za Kiutumishi.
Kamanda Gariyamoshi Amesema Ili Kuhakikisha Tabia Za Uovu Zinatoweka Miongoni Mwa Watumishi Wa Jeshi Hilo Ni Vema Wananchi Wakashiriki Kutoa Taarifa Kwa Kupiga Simu Au Kufika Katika Ofisi Za Jeshi Hilo Wilaya Ili Hatua Zichukuliwe Haraka Kwa Wanaokwenda Kinyume.
Kauli Ya Kamanda Huyo Imekuja Ikiwa Ni Siku Chache Tangu Mkuu Wa Wilaya Ya Ludewa Andrew Tsere Kulaani Kitendo Cha Askali Wa Kituo Cha Polisi Mlangali Kuwalaza Watu Wanaofikishwa Kituoni Hapo Na Kuwatoza Fedha Zilizo Kinyume Na Maadili Ya Kazi Yao Ambapo Kamanda Huyo Ameahidi Kuwachukulia Hatua za kisheria Askali Waliohusika Na Tukio Hilo.
Kamanda GariYaMoshi Amesema Jeshi Hilo Litaendelea Kutoa Elimu Kwa Askali Wake Juu Ya Utendaji Kazi Ili Kusitokee Tena Na Malalamiko Ya Wananchi Kuhusiana Na Askali Huku Akitoa Wito Kwa Wananchi Kuendelea Kuonesha Ushirikiano Kwa Jeshi Hilo Katika Kuwafichua Waharifu.
No comments:
Post a Comment