Wananchi Wa Kijiji Cha Ikando Wilayani Njombe Wameitaka Serikali Kuboresha Miundombinu Ya Barabara Na Afya Ili Kuwanusuru Wamama Wajawazito Wasitozwe Faini Ya Elfu 50 Wakijifungulia Njiani Wakati Wakienda Katika Zahanati Ya Kijiji Cha Ibumila.
Rai Hiyo Imetolewa Na Wananchi Wa Kijiji Cha Ikando Wilayani Njombe Wakati Wakizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Changamoto Zinazowakabili Ikiwemo Tatizo La Kusafiri Umbali Mrefu Wa Kilomita Tano Kufuata Huduma Za Matibabu Zahanati Ya Ibumila.
Wamesema Kero Hiyo Imemufikia Mbunge Wa Lupembe Joramu Hongori Kupitia Mkutano Wake Uliofanyika Augost 8 Mwaka Huu Na Kumpatia Kero Mbalimbali Ikiwemo Manesi Wa Zahanati Ya Ibumila Kuwatoza Faini Elfu 50 Wajawazito Wakijifungulia Njiani Pasipo Kuzingatia Umbali Wanaosafiri .
Wananchi Hao Wamesema Changamoto Nyingine Ni Kukosekana Kwa Madaraja,Maji Na Barabara Rafiki Za Kuunganisha Vijiji Vya Ikando,Ibumila Na Vijiji Vya Kata Ya Igima Vya Igairo Na Lulanzi Ili Kupata Urahisi Wa Kusafirisha Wagonjwa Kuelekea Hospitali Ya Kibena Pamoja Na Mazao Hususani Msimu Wa Masika.
Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Ikando Kata Ya Kichiwa Isack Mwinami Amekili Kuwepo Kwa Tatizo La Kukosekana Kwa huduma Ya Afya Kwenye Kijiji Chake Na Kusababisha Akina Mama Wajawazito Kujifungulia Njiani Na Wakifika Kwenye Zahanati Ya Kijiji Cha Jirani Kuwa Toza Faini Ya Elfu 50 Tatizo Lililokuwepo Hapo Hawali Lakini Siyo Kwa Sasa.
Mwinami Amesema kutokana Na Kuwepo Kwa Tatizo La Kukosekana Kwa Huduma Za Afya Kwenye Kijiji Hicho Jitihada Zimeanza Za Ujenzi Wa Zahanati Ya Kijiji Ili Kurahisisha Huduma Za Afya Kwa Wananchi Huku Akisema Zahanati Iliyopo Inatatizo La Kukosa Dawa Na Kusababisha Wagonjwa Kununua Kwenye Maduka Ya Watu Binafsi.
No comments:
Post a Comment