Umoja Wa Wauzaji Wa
Maduka Ya Dawa Mjini Njombe
UWAMADANJO Leo Umefanikiwa
Kuteuwa Viongozi 10 Wa Muda Ambao
Watasikiliza Kero Za Wanaumoja Huo Na Kuziwasilisha Sehemu Husika Kwaajili Ya
Kupatiwa Ufumbuzi.
Akizungumza Na Uplands Fm
Mara Baada Ya Kufanyika Kwa Kikao Cha Kufanya Uteuzi Huo Mwenyekiti Aliyeteuliwa
Paul Masasi Amesema Lengo La Umoja Huo Ni Pamoja Na Kuboresha Huduma Za Utoaji Dawa Kwa Kila Muuzaji Na
Kudhibiti Uuzwaji Dawa Kiholela.
Bwana Masasi Amesema Umoja
Huo Utahakikisha Unafuatilia Baadhi Ya
Wamiliki Wa Maduka Na Wauzaji Wake
Kuhakikisha Wanakuwa Na Vyeti Halali
Na Siyo Vya Kugushi Pamoja Na
Dawa Ambazo Zimesajiliwa Kisheria
Ambapo Kinyume Na Sheria Uongozi
Utachukua Hatua Za Kufikisha Kwa Mfamasia .
Kwa Upande Wake Muwakilishi Wa Baraza La Famas Ambaye
Pia Ni Mfamasia Wa Halmasahuri Ya Mji Wa Njombe Simon Kwama Amesema
Wamiliki Wa Maduka Ya Dawa
Wanatakiwa Kuzingatia Kanuni Na Sheria Kwa Mujibu Wa Usajili Wa Duka
Lake Ikiwemo Kutochanganya Maabara Na
Duka La Dawa Sehemu Moja.
Mfamasia Huyo Amesema
Kuundwa Kwa Umoja Wa Wauzaji Wa Dawa Mjini Njombe Kutasaidia Miongoni Mwao Kuondokana Na Ukiukwaji Wa Kuuza Dawa Hizo Na Kutaka Wamiliki Wa Maduka Hayo Kuzingatia Kanuni Na
Sheria Walizopewa Kwa Mujibu Wa Leseni Zao.
Baadhi Ya Wamiliki Wa Maduka
Walioshiriki Kwenye Kikao Hicho Kilichofanyikia Ukumbi Wa Miliam Hotel Wamesema Umoja Huo Utawasaidia Kutatua
Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Kudhibiti
Wanauza Dawa Kwenye Maduka Ya Bidhaa Nyingine Za Vyakula Na Kuwasilisha Kero
Zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment