Wamiliki Na Madereva Wa Vyomba Vya Moto Mjini Njombe Wametakiwa Kuondoa Uzemba Wakati Wakiwa Barabarani Na Kuacha Kuendesha Chombo Cha Moto Wakiwa Hawana Uwezo Wa Kuendesha Kwenye Barabara Kuu Na Kufanyia Matengenezo Vyombo Vyao.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Diwani Wa Kata Ya Njombe Mjini Agrey Mtambo Akiwa Miongoni Mwa Mashuhuda Wa Tukio La Ajali Iliyotokea Majira Ya Saa Kumi Na Mbili Na Dakika 45 jioni Ya Jana Augost 23 Katika Eneo La Njia Panda Ya Magereza Ambapo Gari Yenye Namba Za Usajiri T 407 CJM yenye rangi nyeupe ililigonga ubavuni Gari lenye namba T 995 CUX .
Bwana Mtambo Amesema Matukio Ya Ajali Yamekuwa Yakitokea Kutokana Na Uzemba Wa Baadhi Ya Madereva Wakiwa Barabarani Ambapo Ametolea Mfano Wa Ajali Iliyotokea Jana Jioni Katika Eneo La Njia Panda Ya Magereza Ambayo Imesababishwa Na Dereva Aliyekuwa Akitokea Barabara Ya Magereza Kuelekea Mjimwema Na Kuligonga Gari Lililokuwa Likitokea Barabara Ya Songea -Njombe.
Awali Wakizungumza Na Uplands Fm Baadhi Ya Mashuhuda Wa Tukio La Ajali Hiyo Wamesema Uzemba Wa Madereva Ndiyo Chanzo Kikubwa Cha Ajali Za Barabarani Ambapo Katika Ajli Hiyo Haikusababisha Kifo Wala Majeruhi Wowote Huku Wakipongeza Jeshi La Polisi Kwa Kufika Kuimarisha Usalama Wa Raia Katika Eneo La Tukio Lilipotokea.
Jeshi La Polisi Mkoani Njombe Limekuwa Likitoa Elimu Ya Usalama Wa Barabarani Kupitia Uplands Fm Kila Siku Ya Juma Tano Na Kwenye Mikutano Mbalimbali Ya Hadhara Lakini Bado Matukio Ya Ajali Yameendelea Kujitokeza Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe.
No comments:
Post a Comment