Mwenyekiti
wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akiongea
na Wapiga gofu wa klabu hiyo walioondoka Leo (jana) Jijini Dar es salaam
wakati akiwatakia heri katika mashindano ya Moshi open na Tanzania Open
yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro na Arusha.
Mwenyekiti
wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwapa
mkono wa heri Wapiga gofu wa klabu hiyo walioondoka Leo (jana) Jijini
Dar es salaam kuelekea katika mashindano ya Moshi open na Tanzania Open
yanayatarajiwa kuanza hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro na Jijini
Arusha.
Wapiga
golf wa Klabu ya Lugalo wakifanya mazoezi ya Mwisho kabla ya kuondoka
Leo (jana) Jijini Dar es salaam kuelekea katika mashindano ya Moshi
open na Tanzania Open yanayotarajiwa kufanyika hivi Karibuni Mkoani
Kilimanjaro na Arusha.
Na Selemani Semunyu,JWTZ
Timu
ya golf ya Jeshi ya Lugalo imetakiwa kuhakikisha inawapa raha wanachama
wake akiwemo Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi
Jenerali davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya Moshi
Open mashindano yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael
Luwongo wakati akiongea na Wachezaji hao katika mazoezi yao ya Mwisho
katika Klabu ya Lugalo Jijini Dar es Salaam kabla ya Kuondoka kuelekea
Moshi.
"Hakuna
sababu kwa Timu ya Jeshi iliyofanya mazoezi kwa muda Mrefu ikashindwa
kirahisi katika Mashindano kama haya ambayo tuliwahi kuchukua ubingwa
kiukweli wapeni raha wanachama wenu" Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Aliongeza
kuwa Wanachama wa Lugalo akiwemo Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara
hawahitaji kitu kingine zaidi ya Furaha ya Ushindi ambayo watakuwa
wanaifuatilia hivyo ni Jukumu la wachezaji hao kuhakikisha wanakamilisha
Furaha hiyo.
Pia
aliwataka wanachama wa Golf kuhakikisha wanamtuma kazi ili kuhakikisha
mafaninio makubwa yanapatikana ikiwemo kuboresha Uwanja wa Golf wa
Lugalo ambao ni Uwanja uliojengwa na wazalendo kuwa Bora na kuhamasisha
Mashindano mengi ya Kimataifa kuandaliwa katika Uwanja huo.
Mwenyekiti
huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni aliahidi kuboresha Klabu hiyo na
kuifanya kuwa ya kisasa zaidi na Kuwa kiwanja bora Afrika Mashariki na
kuwataka watu wote kujitokeza kushiriki katika mchezo huo kwani ni
mchezo unaokubalika kwa rika zote.
Kwa
upande wake Kapteni wa Timu hiyo Kapten Kassim Usitambe alisema Mara
baada ya Mashindano hayo watakayoshiriki wakiwa ni wachezaji Tisa kutoka
klabu ya Lugalo wataelekea Mkoani Arusha kwa mashindano ya Tanzania
Open.
Kwa
upande wake mmoja wa wapiga Gofu hao Amina Hamisi aliahidi kurejea na
ushindi katioka mashindano hayo ili kutoa zawadio kwa mwenyekiti mpya
ikiwa ni siku chache tu baada ya kuteuliwa kushika madaraka hayo.
Timu
hiyo ya Golf iliyoondoka leo (Agosti Nne) itashiriki Mashindano hayo ya
Moshi Open ambayo Klabu hiyo Mwaka 2014 walichukua kikombe
yatashirikisha Wachezaji wote wakiwemo wa Nje sambamba na ya Tanzania
open ambayo wapiga Gofu kutoka Nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment