HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha
,itaokoa sh.mil.516.792 katika mwaka wa fedha 2016/2017,zilizokuwa
zikipotea katika makusanyo ya ushuru wa mchanga,machinjio na stend
kutokana na udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya mawakala.
Awali halmashauri hiyo ilikuwa
ikitumia mawakala kukusanya ushuru wa vyanzo hivyo vya mapato na
kusababisha upotevu huo wa fedha .
Akitoa ufafanuzi juu ya suala
hilo,mjini Kibaha,mwenyekiti wa halmashauri ya Mji huo ,Leonard Mloe
,alisema aligundua kuwepo kwa udanganyifu huo hivyo kuamua kuagiza
makundi ya madiwani kwenda kufuatilia.
“Baada ya kuwaagiza madiwani hao
kufanya uchunguzi ndipo kulipobainika kweli kulikuwa na upotevu mkubwa
wa fedha ambazo zilikuwa zikifaidisha mawakala kuliko
halmashauri”alisema Mloe.
Mloe alielezea kuwa kati ya fedha
hizo zitakazookolewa ni pamoja na mil.335.392 zilizokuwa zikipotea kwa
mwaka kwenye ushuru wa mchanga.
Alisema katika ushuru wa mchanga
walikuwa wakipokea mil.264.608 kwa mwaka ambapo baada ya kutuma madiwani
waligundua watakuwa wakipata mil.600 kwa mwaka.
“Katika ushuru wa stend
,halmashauri ilikuwa ikipokea makusanyo ya sh.mil.320 kwa mwaka baada ya
uchunguzi tumebaini tunapata mil.458 kwa kipindi hicho na kuokoa mil
138 zilizokuwa zikipotea”alisema Mloe.
Mloe alisema upande wa machinjio
walipata mil.25 kwenye tathmini imebainika fedha halisi zinazopatikana
ni mil.68.400 hivyo wameokoa mil 43.400.
Aidha mwenyekiti huyo,alieleza
vyanzo vyote,vya halmashauri hiyo, vibadilike hesabu zake kuanzia sasa
kwani wanahitaji mapato yanayoendana na chanzo cha mapato.
Mloe alisema kuanzia sasa halmashauri hiyo imeanza kutumia vibarua watakaokuwa wanakusanya ushuru wa vyanzo hivyo kwa usimamizi wa watendaji wa halmashauri badala ya mawakala ambao wamebainika sio waaminifu.
“Vibarua hawa watatumiwa ndani ya miezi mitatu na baada ya hapo watakuwa wakibadilishwa ili kuondokana na tatizo la kupotea kwa fedha”alisisitiza Mloe.
Akingumzia kuhusiana na makusanyo
ya mwaka 2015/2016 ,makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Robert
Machumbe,alisema halmashauri ilikisia kukusanya zaidi ya bil.31.836.942
kutokana na vyanzo vyake vya mapato mbalimbali.
Alielezea kuwa halmashauri kwa
robo ya nne inayoishia mwezi juni 2016 imekusanya bil.7.370.215.637 na
kufanya jumla ya mapato yaliyokwisha kukusanywa kwa kipindi cha robo
zote nne kuanzia Julai-Juni 2016 kuwa zaidi ya bil.25.938 sawa na
asilimia 81 ya makisio ya kipindi hicho.
Machumbe alisema halmashauri ya Mji huo imekisia kutumia zaidi ya bil.31.836 kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo
Alieleza katika utekelezaji wa
shughuli zake kwa robo ya nne iliyoishia juni 2016 imetumia
bil.5.950.420 na kufanya jumla ya matumizi kwa julai/juni mwaka huu
kufikia bil.21.614.164 sawa na asilimia 67 ya makisio.
No comments:
Post a Comment