Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, August 3, 2016

POLISI KUBORESHA VITUO VYAKE VYA AFYA.


po1Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
po2
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.Kulia ni Mganga mkuu wa Polisi Dk.Janda Lushina na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Lazaro Mambosasa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) po3Baadhi ya Maofisa wa Polisi ambao ni Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu ndani ya Jeshi la Polisi wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani Dodoma.Mradi huo unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi ……………………………………………………………………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Dodoma
Jeshi la Polisi nchini litaendelea kuboresha vituo vyake vya afya ili kuwawezesha Askari kupata huduma zilizo bora jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi wakiwa na afya pamoja na morali katika kupambana na uhalifu nchini.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki Mkoani Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa  kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini  kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.
 
Kaniki alizitaja juhudi zinazoendelea kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuboresha majengo, kutoa mafunzo kwa watendaji pamoja na kuhakikisha kuwa hospitali za Polisi zinakuwa na vifaa bora kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Wizara ya Afya .
 
Aidha alitoa wito kwa Shirika la JSI-AIDS Free kuongeza wigo wa huduma zake katika vituo vngine ambavyo havijafikiwa na mradi huo hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kila mahali palipo na kituo cha Afya cha Polisi kunakuwepo na mradi huo ambao umesaidia sana askari na watumiaji wengine wa huduma hizo.
 
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania Dk.Beati Mboya alisema lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ili kubaini mafanikio na changamoto zinazovikabili vituo vinavyotekeleza mradi huo ilikuzipatia ufumbuzi.
 
Alisema wanatarajia kufanya tathmini hiyo kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha hakuna ucheleweshaji katika kutoa huduma baada ya kubaini changamoto na kuzifanyia kazi kwa haraka.
 
Naye Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Paul Kasabago alisema kikosi hicho kitaendelea kutoa huduma zilizobora ili kuimarisha afya za Askari na familia zao kote nchini licha ya kukabiliwa na upungufu wa wahudumu wa Afya.
 

No comments:

Post a Comment