Afisa
Mipango wa Kampuni Old East International Ephrahim Moses Mwano akiwa
anaonyesha Aina ya Wino wa Crown ambao wanatengeneza hapa nchini,Katika
maonyesho ya wakulima na wafugaji Katika viwanja vya nanenane Njiro
Jijini Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Old East International Moses Mwano akiwa anazungumza
na wateja waliotembelea banda hilo katika Maonyesho yanayoendelea
katika Viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
Meneja
mauzo wa Kampuni Old East International akiwa anamfafanulia mteja juu
ya Crown Cartridge,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya
Taso nanenane.
Na Woinde Shizza,Arusha.
Wito
umetolewa kwa Watanzania watumie na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na
kupatikana ndani ya nchi badala ya kuzipa kipaumbele bidhaa za nje ya
nchi.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Old East International ndugu Moses Mwano
,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane njiro
Jijini Arusha.
Mwao
amesema kuwa Watanzania wengi wanathamini bidhaa zinazoingia nchini
kutoka nje ya nchi,ambazo baadhi hazina kiwango cha ubora unaotakiwa kwa
mtumiaji.
Mkurugenzi
huyo wa Kampuni ya Old East International amesema kuwa kampuni hiyo ni
ya Kitanzania ,imesajiliwa na ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania
wao ni wawekezaji wa ndani,wanahusika kutengeneza wino wa kuchapia
unaofahamika kwa jina la Crown Cartridge.
Kwa
upande wake Mwano amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya
Tanzania Dokta John Magufuli,katika jitihada zake za kuifanya Nchi kuwa
ya Viwanda.
Sambamba
na hayo amewaasa Watanzania watengeneze na kuingiza Bidhaa zenye
kukidhi ubora na viwango ,huku akimalizia na msemo usemao " kizuri cha
jiuza kibaya chajitembeza akimaanisha kuwa ukitengeneza bidhaa nzuri
yenye kukidhi viwango na ubora unaohitajika wateja watafurahiwa nayo.
No comments:
Post a Comment