MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT NCHIMBI AKIZUNGUMZA NA KUONEKANA KUKELWA NA UCHAFU ULIOPO KWENYE VIZIMBA NJOMBE MJINI IKIWA NI ENEO LA MAKAO MAKUU YA MKOA WA NJOMBE.
HII NDIYO HALI YENYEWE ANAYOIPIGIA KERERE MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT NCHIMBI NA HAPA NI MTAA WA MELINZE
HUU NDIO MRUNDIKANO WA UCHAFU KWENYE VIZIMBA MITAA KARIBU YOTE YA NJOMBE MJINI HALI IKO HIVI. N
Na Michel Ngilangwa -Njombe
Licha Ya Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kuwa Miongoni Mwa Halmashauri Zilizopata Tuzo Ya Ushindi Katika Mashindano Ya Afya Na Usafi Wa Mazingira Nchini ,Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Ametoa Onyo Kwa Halmashauri Hiyo Kwamba Inakabiliwa Na Tatizo La Uchafu Na Harufu Mbaya Inayotokana Na Mkusanyiko Wa Taka Zilizopo Kwenye Vizimba Mjini Hapa.
Akizungumza Na Wakuu Wa Wilaya ,Wakurugenzi,Wenyeviti Wa Halmashauri Na Baadhi Ya Wananchi Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amemtaka Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Iluminata Mwenda Kuhakikisha Anasimamia Zoezi La Uondoaji Wa Taka Kwenye Vizimba Vilivyopo Katika Maeneo Mbalimbali Ya Sokoni Na Kwenye Makazi Ya Watu.
Hatua Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Nchimbi Kumuagiza Mkurugenzi Huyo Imefuatia Halmashauri Hiyo Kupewa Tuzo Ya Kikombe Na Pikipiki Moja Kwaajili Ya Ushindi Wa Mashindano Ya Afya Na Usafi Wa Mazingira Licha Ya Mji Wake Kuwa Na Harufu Mbaya Inayotokana Na Uchafu Wa Vizimba Ambavyo Haviondolewi Takataka Zake Kwa Muda Murefu.
Alphan Ngulo Ni Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Joshoni Mjini Njombe AAkizungumza Na Uplands Fm Hapo Jana Amesema Tatizo La Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kushindwa Kuondoa Takataka Kwenye Vizimba Limekuwa Ni La Muda Mrefu Licha Ya Viongozi Wa Mitaa Kuwapatia Taarifa Za Kuwepo Kwa Taka Hizo Ikiwemo Kizimba Cha Soko La Joshoni Ambacho Kina Takribani Miezi Sita Hakijafanyiwa Usafi.
Kwa Upande Wake Wananchi Mjini Njombe Wamelalamikia Kuwepo Kwa Tatizo La Kushindwa Kuondolewa Kwa Taka Kwenye Vizimba Kwa Muda Mrefu Huku Wakitolea Mfano Kizimba Cha Mtaa Wa Sido Nyuma Ya Uwanja Wa Sabasaba,Nationalhousing,Buguruni Na Maeneo Mengine Ambayo Yanakabiliwa Na Changamoto Ya Uchafu Licha Ya Kutozwa Hela Ya Uchafu.
.........................................................................
No comments:
Post a Comment