Saturday, August 6, 2016
RC NJOMBE AAGIZA KUWASAKA, KUFUNGIA BAR ZINAZOUZA MABARMED
MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI
Wakurugenzi Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Wametakiwa Kufanya Oparesheni Ya Kuwakamata Na Kuwachukulia Hatua Za Kisheria Baadhi Ya Wamiliki Na Waajili Wa Wafanyakazi Wa Biashara Za Pombe Ikiwa Ni Pamoja Na Kuzifunga Bar Zote Zenye Mabamed Ili Kupunguza Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi Mkoani Hapa Kwa Kipindi Hiki Cha Utawala Wa Rais Wa Awamu Ya Tano .
Agizo Hilo Limetolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Wakati Akizungumza Na Wakurugenzi Wa Kutoka Halmashauri Sita Za Mkoa Wa Njombe Na Kutaka Wakurugenzi Hao Kushirikiana Na Taasisi Nyingine Zisizo Za Kiserikali Kutokomeza Tabia Ya Baadhi Ya Waajili Wa Wafanyakazi Wa Bar Ambao Wanachukuliwa Sehemu Mbalimbali Kwa Lengo La Kuwauza Kigono.
Aidha Dkt Nchimbi Ametolea Mfano Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kwamba Kuna Bar Ambazo Wamiliki Wake Wameajili Wafanyakazi Wa Kuuza Pombe Hizo Na Miili Yao Pasipo Wao Kukusudia Huku Mameneja Wengine Wakiwaweka Kwenye Mazingira Hatarishi Wafanyakazi Hao Kwa Kuwataka Wafanye Matendo Maovu Ya Kwenye Madanguro Yanayoashilia Kueneza Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi.
Dkt Nchimbi Ametaka Kufungiwa Kwa Bar Hizo Na Kuwachukulia Hatua Kali Mameneja Wanaoendekeza Biashara Ya Ngono Kwa Kuwauza Mabinti Wa Bar Baada Ya Wakurugenzi Hao Kufanya Msako Wa Mabamedi Wanaojihusisha Na Vivutio Vya Ngono Na Kusababisha Maambukizi Hayo Kuendelea Kueneo Kwa Mkoa Wa Njombe Ambapo Wanatakiwa Kuvunja Mitandao Ya Kueneza Maambukizi Hayo.
Katika Hatua Nyingine Dkt Nchimbi Ametaka Wananchi,Wadau Wa Elimu, Jeshi La Polisi Kwa Kushilikiana Na Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa Nchini Takukuru Mkoa Wa Njombe Kuwa Karibu Na Maeneo Ya Shule Za Msingi Ili Kuwabaini Baadhi Ya Walimu Wenye Mahusiano Ya Kingono Na Wanafunzi Na Kuwachukulia Hatua Kali Za Kisheria Akiwemo Mwalimu Anayetuhumiwa Kuwa Na Mahusiano Ya Kingono Na Wanafunzi 12 Wilayani Ludewa.
Agizo Lingine La Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Ni Pamoja Na Maafisa Elimu Kutumia Baiskeli Kuzifikia Shule Wanazozisimamia Endapo Halmashauri Zao Zitakosa Mafuta Ya Kuweka Kwenye Magari Na Kuwatimua Walimu Wenye Tabia Ovu Shuleni Za Kingono Na Wanafunzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment