HIVI NI VYOO VYA MUDA WANAVYOTUMIA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI IDINDILIMUNYO BAADA YA KUTITIA VYOO VYA AWALI MWEZI MACH MWAKA HUU
HIVI NI VYOO VILIVYOTITIA MWEZI MACHI MWAKA HUU KATIKA SHULE YA MSINGI IDINDILIMUNYO
WAZAZI WA KIJIJI CHA IDINDILIMUNYO WAKALAZIMIKA KUANZA ZOEZI LA KUCHIMBA SHIMO NA KUANZA UJENZI WA VYOO VYA KISASA NA LILIPOKUJA ZOEZI LA UCHANGIAJI MADAWATI WAKAGOMA KUCHANGIA HADI WAKAMILISHI MRADI HUU WA VYOO VILIVYO SALIA KUWEKA MILANGO NA KUPAKWA RANGI
HAPA NI JIKONI WANAKOPATIWA CHAKULA WANAFUNZI WA SHULE HIYO
HIVI NDIVYO VYOO WANAVYOTUMIA KWA SASA KATIKA SHULE YA MSINGI IDINDILIMUNYO
VYOO WALIVYOJENGA AMBAVYO BADO HAVIJAANZA KUTUMIKA VINA MASINKI NA KILA KITU KASORO MILANGO WANASEMA WANAENDELEA NA JITIHADA ZA KUKAMILISHA
HIVI NI VYOO VYA ZAMANI VILIVYOHARIBIKA KATIKA SHULE HIYO
Wananchi Wa Kijiji Cha Idindilimunyo Wilaya Ya Wanging'ombe Mkoani Njombe Wametishia Kugoma Kuchangia Michango Ya Madawati Ili Kutekeleza Agizo La Rais Magufuli Kwa Madai Kuwa Hawawezi Kuchangia Miradi Miwili Kwa Wakati Mmoja Nakwamba Hadi Wakamilishe Ujenzi Wa Vyoo Kwaajili Ya Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Idindilimunyo Kufuatia Vyoo Vya Zamani Kutitia Mwezi Mach Mwaka Huu.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Wananchi Wa Kijiji Hicho Wakati Wa Mkutano Wa Hadhara Uliofanyika Jana Na Kusema Kuwa Hawawezi Kuchangia Madawati Kwa Kipindi Hiki Ikiwa Wanaendelea Na Ujenzi Wa Vyoo Vya Kisasa Kwaajili Ya Wanafunzi Hao Nakwamba Dhamira Yao Ni Kutaka Kuweka Mazingira Mazuri Ya Wanafunzi Katika Kuelekea Kipindi Cha Mvua.
Aidha Wananchi Hao Wamesema Kuwa Siyo Kwamba Wanakataa Kuchangia Madawati Hayo Bali Jitihada Zao Wanazielekeza Kwenye Kipaumbele Chao Kikubwa Cha Tatizo La Wanafunzi Kukosa Vyoo Kwani Hadi Sasa Wanatumia Vya Muda Vilivyoezekwa Kwa Majadi Ambapo Ili Kuepukana Na Tatizo La Mlipuko Wa Magonjwa Ya Kipindupindu Imewalazimu Kukamilisha Ujenzi Huo Mwaka Huu.
Akizungumza Mara Baada Ya Kumalizika Kwa Mkutano Wa Hadhara Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Idindilimunyo Goden Kasanga Ameutupia Lawama Uongozi Wa Halmashauri Ya Wanging'ombe Kwa Kushindwa Kulichukulia Uzito Swala La Kukosekana Kwa Vyoo Katika Shule Hiyo Huku Akisema Serikali Ya Kijiji Hicho Inaungana Na Wananchi Kutochangia Madawati Kwa Mwaka Huu.
Kasanga Amesema Kuwa Hadi Sasa Serikali Ya Kijiji Kwa Kushilikiana Na Wananchi Wake Wamekamilisha Ujenzi Wa Matundu 16 Ya Vyoo Vya Kisasa Ambavyo Vimebakia Kuweka Masink Vilivyo Gharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 20 Ikiwa Halmashauri Kupitia Idara Ya Elimu Haijashiliki Kupeleka Msaada Wowote Kunusuru Afya Za Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Idindilimunyo Ambao Vyoo Vyao Vilititita Mwezi Mach Mwaka Huu.
Uplands Fm Imeshuhudia Vyoo Vya Muda Vinavyotumiwa Na Wanafunzi Kwa Sasa Vikiwa Vimejengwa Kwa Majani Baada Ya Vyoo Vya Zamani Kutitia Jambo Lililowalazimu Wananchi Na Serikali Yao Kuanza Mara Moja Jitihada Za Ujenzi Huo.
No comments:
Post a Comment