MBUNGE WA JIMBO LA MAKAMBAKO AKIKABIDHI MSAADA HUO KWA MAASKALI MAGEREZA WA GEREZA LA NJOMBE KWAAJILI YA WAFUNGWA
HAWA NI ASKALI MAGEREZA WA NJOMBE WAKIWA WAMESHIKA MABLANKETI HAYO YALIOTOLEWA NA MBUNGE WA MAKAMBAKO
blanketi 40 baada ya kupokelewa zimehifadhiwa kwaajili ya kuchukuliwa na wafungwa wa gereza la Njombe
Kaimu Mkuu Wa Gereza Wilaya Ya Njombe Alfred Nyakimbo Matu Akishukuru Kwa Niaba Ya Wafungwa hao
HIZI NI NYUNGO ZA VING'AMUZI VILIVYOTOLEWA NA MBUNGE WA MAKAMBAKO DEO SANGA MAARUFU KAMA JA PEOPLE KWA WAFUNGWA WA GEREZA LA NJOMBE
Mbunge Wa Jimbo La Makambako Deo Sanga Amekabidhi Msaada Wa Blanketi 40 Na Ving'amuzi Viwili Kwa Wafungwa Wa Gereza La Njombe Wenye Zaidi Ya Shilingi Milioni Moja Ili Kuwaokoa Na Baridi Gerezani Humo.
Hatua Ya Mbunge Wa Jimbo La Makambako Deo Sanga Maarufu Kwa Jina La Ja People Kukabidhi Msaada Huo Imekuja Baada Ya Kutembelea Gereza Hilo Hivi Karibuni Na Kupokea Matatizo Lukuki Ikiwemo Upungufu Wa Blanketi Na Ving'amuzi.
Bwana Sanga Amesema Kutembelea Gereza Hilo Ni Wajibu Wake Akiwa Mbunge Ambapo Msaada Huo Ni Utekelezaji Wa Ahadi Yake Aliyoitoa Hivi Karibuni Kwa Wafungwa Hao Baada Ya Kuelezwa Kuwa Baadhi Yao Wapo Gerezani Kwa Kukosa Kulipa Faini Kuanzia Elfu Hamsini hadi Laki Mbili.
Bwana Sanga Ametumia Fursa Hiyo Kuwaomba Wadau Wengine Wa Maendeleo Kujitokeza Katika Gereza Hilo Kutoa Misaada Mbalimbali Kwa Wafungwa Ikiwemo Kusaidia Walioko Gerezani Kwa Kukosa Fedha Kwaajili Ya Kulipa Faini Walizopangiwa Na Mahakama.
Kaimu Mkuu Wa Gereza Wilaya Ya Njombe Alfred Nyakimbo Matu Ameshukuru Kwa Msaada Uliotolewa Na Mbunge Huyo Na Kuwaomba Wadau Wa Maendeleo Kujitokeza Kusaidia Wafungwa Waliopo Kwenye Gereza Hilo Huku Akiwatoa Hofu Baadhi Ya Wananchi Wenye Imani Potofu Kwamba Wakifika Gerezani Hapo Nao Watafungwa.
Sp Matu Amesema Mablanketi Hayo Yatasaidia Katika Kujihifadhi Na Baridi Kwa Wafungwa Wa Gereza Hilo Na Kutaka Wenye Nia Njema Kufika Kuwasaidia Misaada Mbalimbali Ambayo Itakuwa Haina Masharti Yoyote Yatakayotolewa Kwa Wafungwa Na Wasimamizi Wa Gereza Hilo.
Msaada Huo Uliotolewa Na Mbunge Wa Jimbo La Makambako Deo Sanga Maarufu Kwa Jina La Ja People Unatoa Mfano Wa Kuigwa Kwa Taasisi Za Serikali,Watu Binafsi Na Viongozi Mbalimbali Kutekeleza Wajibu Wa Kutembelea Makundi Maalumu Kwaajili Ya Kutoa Misaada Na Kuwa Mfano Kwa Wananchi Kutembelea Makundi Hayo .
No comments:
Post a Comment