LUKELO MSHAURA AFISA HABARI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NJOMBE
HIKI NDIO KITUO CHENYEWE CHA KUTOLEA MAFUNZO KWA WAKULIMA WILAYANI NJOMBE
Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Kupitia Programu Ya MIVARF Inakarabati Kituo Cha Mafunzo Ya Kuzuia Upotevu Wa Mazao Ya Mbogamboga Na Matunda Lengo Kuwezesha Wakulima Kuzuia Upotevu Na Kuongeza Thamani Ya Mazao Na Kipato Cha Mkulima .
Afisa Habari Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Lukelo Mshaura Amesema Kupatikana kwa mradi huo Kunatokana Na Jitihada Za Halmashauri Hiyo Kuandaa Maandiko Mbalimbali Ya Uwekezaji Wa Miradi Ya Maendeleo Kwa Lengo La Kusaidia Wananchi Na Kuongeza Mapato Ya Halmashauri.
Bwana Mshaura Amesema Mradi huo Unaofadhiliwa Na Programu Ya Mivarf Ni Muendelezo Wa Mradi Mwingine Wa Kuimarisha Zao La Mnyororo Wa Mahindi kupitia taasisi ya Uongozi Na Maendeleo Ya Ujasiliamali Unaotekekezwa Katika Vijiji 13 Kwa Kata Za Ninga, Ikuna, Na Kichiwa Wilayani Njombe.
Amesema Kazi Kubwa Inayofanywa Na MIVARF Kwa Kushirikiana Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ni Kuwajengea Uwezo Wakulima Na Vikundi Vya Uzalishaji Ikiwemo AMCOS Na Kuwaunganisha Kwenye Masoko Kwa Zao La Mnyororo Wa Thamani Lililochaguliwa Na Wadau Wa Kilimo Ambalo Ni Mahindi.
Amesema Kituo Hicho Kitakuwa Na Uwezo Wa Kuchukua Watu 40 Kwa Wakati Mmoja Ukarabati Wake Utaghalimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 74 , Unatekelezwa Kwa Awamu Mbili , Ikiwemo Ukarabati Uliopo Kukamilishwa Na Usimikaji Mitambo Iliyopo Kwenye Mchakato Wa manunuzi .
Amesema Kituo Hicho Kitahudumia Wakulima , Mkoa Wa Njombe Ambao Wazarishaji Wa Mazao Ya Matunda Na Mbogamboga Hususani Nyanya Na Kitatoa Fursa Kwa Vikundi Kupata Mafunzo Ya Stadi Za Usindikaji Mazao Na Kusaidia Kupunguza Upotevu Wa Mazao Na Kuongeza Thamani Na Kipato.
No comments:
Post a Comment