MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD FRANZ MWALONGO AKIZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA NJOMBE MJINI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE PUDENCIANA PLOTAS AKIWA NA VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA NJOMBE MJINI
HAWA WAFANYABIASHARA WA NJOMBE WAKISIKILIZA KWA UMAKINI HOTUBA YA MBUNGE WA NJOMBE MJINI EDWARD FRANZ MWALONGO
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA NJOMBE ONESMO BENEDICT WA KULIA AKIWA NA KAIMU WAKE WAKIJADILIANA JAMBO UKUMBI WA TURBO
MWANYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA NJOMBE ONESMO BENEDICT AKIZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA MBELE YA MBUNGE YEYE ANASEMA HUWA WANAOMBA KUKUTANA NA MKURUGENZI USO KWA USO NA MKURUGENZI LAKINI AMEKUWA AKIPIGA CHENGA SASA WANAHITAJI KUKUTANA NAYE WAFANYE MAZUNGUMZO JUU YA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.
MWALONGO EDWARD AKIWA UKUMBI WA TURBO NJOMBE MJINI
Serikali Imetenga Kiasi Cha Shilingi Milioni Mia Nane Katika Bajeti Ya Mwaka 2016/2017 Kwaajili Ya Kukarabati Hospitali Ya Mkoa Wa Njombe Kibena Ambapo Ukarabati Wake Unatarajia Kufanyika Mara Baada Ya Fedha Hizo Kufika Ili Kupunguza Changamoto Ya Uchakavu Wa Miundombinu Mbalimbali Ya Hospitali Hiyo.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mbunge Wa Jimbo La Njombe Mjini Edward Franz Mwalongo Wakati Akizungumza Na Wafanyabiashara Wa Njombe Mjini Na Kusema Kuwa Wafanyabiashara Wanatakiwa Kutambua Kuwa Serikali Inamalengo Ya Kuboresha Miundombinu Mbalimbali Ya Kijamii Ikiwemo Ukarabati Wa Sehemu Za Afya.
Aidha Mwalongo Amesema Serikali Inaendelea Na Jitihada Za Kupeleka Mradi Wa Maji Katika Hospitali Ya Kibena Ambapo Mradi Huo Umedaiwa Utadumu Kwa Muda Wa Mwaka Mmoja Kukamilika Kwake Na Kipaumbele Cha Maji Hayo Kufikishwa Kitakuwa Kwenye Hospitali Na Eneo La Chuo Cha Nurssing Kibena.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara Njombe Mjini JWT Onesmo Benedict Amesema Wafanyabiashara Hao Wanakabiliwa Na Changamoto Ya Serikali Kuwatumia Wafanyabiashara Wa Mikoa Ya Nje Kusambaza Vifaa Vya Ujenzi Ikiwemo Saruji,Nondo Na Mali Nyingine Za Kujengea Kutochukuliwa Njombe Licha Ya Badhaa Hizo Kuwepo Madukani.
Nao Wafanyabiashara Waliokuwepo Kwenye Mkutano Huo Wamelalamikia Kuwepo Tatizo La Uchafu Iliopo Kwa Baadhi Ya Maeneo Na Kusema Wataalamu Wa Afya Hakuna Kazi Wanayoifanya Na Kumuomba Mbunge Kutilia Mkazo Swala La Usafi, Uharibifu Wa Miundombinu Ya Barabara Huku ZIlizolimwa Kutomwagiwa Maji.
No comments:
Post a Comment