Thursday, August 18, 2016
IDARA ZA AFYA ZA TAKIWA KUWA NA TAARIFA SAHIHI ZA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
WA UPANDE WA KULIA NI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAHU,WA PILI KUTOKA KULIA NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI NA WA TATU KUTOKA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI WAKIWA KWENYE KIKAO CHA AFYA YA MSINGI CHA MKOA WA NJOMBE
HAWA NI WATAALAMU WA AFYA WA KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA NJOMBE
MKURUGENZI WILAYA YA WANGING'OMBE BI.KIWANUKA AKIWA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE ANTONY MAHWATA
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ALLY KASINGE ALIYEVAA MIWANI WA KWANZA NA WA PILI NI MKURUGENZI HALMASHAURI YA MAKAMBAKO PAUL MALALA WAKIWA NA KIKOSI CHA JESHI LA POLISI KWENYE KIKAO CHA AFYA YA MSINGI
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amezitaka Halmashauri Kupitia Idara Za Afya Kuhakikisha Zinatafuta Taarifa Sahihi Za Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi Pamoja Na Kutatua Changamoto Zilizopo Na Namna Ya Kuzitatua.
Akizungumza Wakati Wa Kufungua Kikao Cha Kamati Ya Afya Ya Msingi Akiwa Ni Mwenyekiti Wa Kikao Hicho Dkt Nchimbi Amesema Haikubaliki Mkoa Wa Njombe Unaopewa Sifa Kwa Kushinda Mashindano Mbalimbali Kitaifa Na Kikanda Ukaongoza Kwa Maambukizi Ya Ukimwi Na Kutaka Wadau Na Wataalamu Kutafuta Suruhisho Lake.
Dkt Nchimbi Amesema Kila Halmashauri Kupitia Idara Za Afya Zinatakiwa Kuandaa Mikakati Mbalimbali Ya Kufikia Maambukizi Sifuri Ifikapo Mwaka 2020 Na Maambukizi Ya Asilimia 3 Ndani Ya Mwaka Huu Kwa Kupata Takwimu Zilizo Sahihi Kwa Kuweka Kitu Cha Pekee Katika Sekta Ya Afya Na Siyo Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Mazoea.
Dkt Nchimbi Bado Amerudia Kauli Yake Ya Kuzifungia Bar Zote Zinazoendesha Biashara Zao Kinyume Na Maadili Kwa Kuwauza Wafanya Kazi Wao Yaani Mabarmed Ambao Wamedaiwa Kuchangia Maambukizi Ya UKIMWI Mkoa Wa Njombe Kutokana Na Uhamisho Wao Wa Mara Kwa Mara Na Kuwaagiza Wakuu Wa Wilaya Kusimamia Zoezi Hilo Wakishilikiana Na Jeshi La Polisi.
Akiwasilisha Taarifa Ya Maambukizi Ya UKIMWI Mkoa Wa Njombe Afisa Ustawi Wa Jamii Mkoa Wa Njombe Bi. Teresia Yomo Amesema Kuna Njia Mbalimbali Ambazo Zinaweza Kuchangia Maambukizi Hayo Ikiwemo Kunyoa Kwenye Saluni,Kutumia Pamoja Vitu Vyenye Nja Kali Huku Akisema Kuna Waraka Ambao Unamuongoza Muajili Kumsaidia Mfanyakazi Kwa Kumpatia Elimu Na Kuwangezea Posho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment