MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ALLY KASINGE AKITOA MAAGIZO KWA MKURUGENZI WA WANGING'OMBE MBELE YA WANANCHI WA KIJIJI CHA MNG'ELENGE
HILI NIN JENGO LA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MNG'ELENGE AMBAYO INAENDELEA NA UJENZI
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE AKIZUNGUMZA NA MKANDARASI NODRICK DANIEL MNG'ONG'O ALIYEJENGA ZAHANATI HIYO NA KUPOKEA FEDHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI NNE BADALA YA ZAIDI YA SHILINGI MILIINI TATU NJE YA MKATABA
AFISA USHIRIKA WILAYA YA WANGING'OMBE GOODSON MTAMA AKIFAFANUA JUU YA CHAMA CHA AMCOS
DKT JAMES LIGWA AKIWA KWA NIABA YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE
HUYU NI MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MNG'ELENGE ALIYEKAIMISHWA KWA MUDA BAADA YA WA ZAMANI KUTENGULIWA NAFASI YAKE YA UONGOZI NA WANANCHI
DIWANI WA KATA YA WANGING'OMBE GEOFREY NYAGAWA AKISHUKURU KWA KUFIKA MKUU WA WILAYA KUTOA UFAFANUZI
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Ally Kasinge ameagiza kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi waliokiuka sheria za kumlipa pesa tasilimu mkandarasi aliyejenga zahanati ya Mng’elenge bila kumuandikia hundi kinyume na sheria.
Bw. Kasinge ametoa maagizo hayo katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mng’elenge Kata ya Wanging’ombe wilayani wanging’ombe wakati akitoa mrejesho kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya ujenzi wa zahanati ya kijii hicho.
Amesema kuwa watumishi wa Halmashauri hiyo wamefanya malipo ya fedha kiasi cha shilingi milioni 15 pasipo kuandika hundi kama sheria inavyowataka.
Kasinge amebainisha mapungufu mengine kuwa ni kufanyika kwa manunuzi ya moja kwa moja bila kufuata sheria za manunuzi na kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 10 ikiwa sheria inawataka kufanya ushindanishi wa manunuzi tofauti na wao walivyofanya.
Diwani Wa Kata Ya Wanging'ombe Wilayani Wanging'ombe Geofrey Nyagawa Amepongeza Wananchi Kwa Jitihada Walizofanya Za Kuwapigia Kelele Viongozi Na Hatimaye Ukweli Umepatikana Na Kutaka Kurudisha Moyo Wa Kushiriki Shughuli Za Maendeleo Kama Zamani.
Zahanati ya kijiji hicho inatarajia kugharimu zaidi ya milioni 90 hadi kukamilika kwake ambapo Halmashauri imechangia kiasi cha milioni 15 huku nguvu za wananchi zikiwa ni zaidi ya milioni 8 na kufikia zaidi ya shilingi milioni 23 hadi ilipo fikia hatua ya upauwaji.
No comments:
Post a Comment