MADEREVA WENZAKE WAKIMPOKEA NJE YA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA MWENZAO ANAYESTAAFU PHED NDALE
HAPA NI BAADHI YA MADEREVA WAKIWA NA AFISA MIPANGO BI. WAZA NA AFISA UTUMISHI AMBAYE NI MGENI RASMI
MADEREVA HAO WAPO KWENYE MAOMBI KABLA SHEREHE HAIJAANZA
WA KWANZA KUTOKA KULIA NI MKE NA DEREVA ALIYESTAAFU MUDA WAKE WA KAZI PHED NDALE WA PILI KUTOKA KULIA NI PHED NDALE ANAYEAGWA WA TATU KUTOKA KULIA NI MGENI RASMI AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI HIYO FRANK EDGAR KOMBA NA WA NNE NI MWENYEKITI WA MADEREVA WILAYA YA NJOMBE PATRICK MFIKWA.
MWENYEKITI WA MADEREVA WA SERIKALI WILAYA YA NJOMBE PATRICK MFIKWA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI
Umoja Wa Madereva
Wilayani Njombe Wametakiwa Kuzingatia
Sheria Na Kanuni Za Udereva Na Maadili Ya Kiutumishi na kuvumilia vikwazo mbalimbali vinavyoweza
kutokea baina ya wakuu wa idara na kuwasilisha malalamiko kwa
mwajili wao.
.Rai hiyo imetolewa na afisa
utumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Frank Edgar Komba wakati akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya
mkurugenzi wa halmashauri hiyo katika hafra fupi ya kumuaga dereva Phed Ndale
aliyestaafu kazi mwezi huu.
Bwana Komba amewasihi
watumishi wastaafu kwamba wanatakiwa kwenda kuishi vizuri na jamii kama walivyokuwa wakiishi wakiwa kazini na kuiendeleza
miradi iliyokwishaibuliwa na siyo
kutumia pesa za mafao ya kustaafu kuanzishia miradi mipya.
Akizungumza mbele ya wana
umoja wa madereva hao dereva aliyekuwa
anaagwa Bwana Phed Ndale amesema
madereva wanaobaki wanatakiwa kuzingatia miiko ya kazi za kiutumishi ili
wasifukuzwe kazi na kuacha ugomvi na wakuu wa idara pindi vikwazo vinapokuwa
vinatokea.
Bwana Ndale Amesema Ameanza
Kazi Serikalini Mwaka 1973 akiwa ametoka kufanya kazi kama
kibarua kwa kipindi cha miaka 13 serikalini
na uvumilivu wake ndiyo uliomsaidia hadi kufikia kustaafu kwake.
Mwenyekiti wa umoja wa
madereva kwa Halmashauri tatu za Njombe, Wanging’ombe na Makambako Luka Malongo ametoa historia ya umoja
huo kwamba ulianzishwa mwaka 2013 wakiwa
32 baada ya kuambiwa wabadilishe leseni kwa lengo la kutatua changamoto
mbalimbali za kila dereva na kusaidiana kwenye shida na raha huku mwenyekiti wa
madereva Wilaya ya Njombe Patrick Mfikwa akisema umoja huo utaendelea
kudumishwa.
No comments:
Post a Comment