Makamu
Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na
mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick
(aliyeshika kipaza sauti) akijibu maswali mbele ya waandishi wa habari
wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle
uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake
kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa
wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi
wengine. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo
inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz
Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akiwasikiliza waandishi wa habari
wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle
uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake
kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa
wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi
wengine.
Washiriki waliohudhuria mkutano huo.
Mkutano
wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle umefanyika jijini
Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt ambapo wadau mbalimbali wa masuala
ya teknolojia walikutana na kujadili matumizi salama ya mtandao. Mambo
makuu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu
Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba, ni
usalama katika matumizi ya mitandao ya teknojia, Usimamizi wa utunzaji
wa data na taarifa za siri na jinsi ya kukabiliana na hasara
zinazotokana na matumizi mabaya ya mtandao yenye kuleta athari kwa
watumiaji. Imeeleza katika mkutano huo kuwa kila mwaka mabilioni ya dola
hutumiwa na taasisi mbalimbali kujiweka salama na athari za kimtandao
ambapo hata hivyo imeelezwa kuwa wezi wanaojinufaisha kupitia teknolojia
kila kukicha wanabuni mbinu mpya za kufanya uharifu kupitia katika
mitandao ikiwemo kuiba taarifa za siri kutoka kwenye makampuni na
taasisi. Taarifa zimebainisha kuwa hivi karibuni wizi wa kimtandao
uliosababisha hasara ya dola za Kimarekani bilioni 300 umefanyika na
kiasi cha dola bilioni100 umefanyika kupitia kadi maalumu za mihamala ya
fedha na malipo, bara la Afrika likiwa moja ya wahanga wa wezi huu wa
kimataifa. Ripoti ya mwaka huu kutoka taasisi za Verizon kuhusiana na
wizi wa kimtandao imebainisha kuwa kuwa wizi wa siri za makampuni ni wa
pili kufanyika baada ya wizi wa fedha japo makampuni mengi hayajawa na
mwamko wa kuwekeza katika kupambana na tatizo hili kubwa ambalo hivi
sasa ni janga la kimataifa. Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya
Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao
duniani, Janusz Nacklicki amesema kuwa mikakati ya kuzuia wizi huu
kuliko athari zinazojitokeza baada ya kuingiliwa katika mtandao na
kuibiwa taarifa za siri za kampuni. Alisema wizi huu wa kimtandao ni
moja ya changamoto inayozikabili taasisi mbalimbali na makampuni ya
biashara na ndio mwanzo wa kutengenezwa bidhaa bandia kwenye masoko na
alisisitiza kuwa utunzaji wa taarifa za siri ni jambo la kwanza la
msingi kwa kampuni Mkutano huo ambao umedhaminiwa za taasisi za Oracle
na CIO Afrika na kuhudhuriwa na watendaji kutoka serikali na taasisi
mbalimbali umetoka na maazimio ya kuhakikisha uwekezaji wa kiteknolojia
unafanyika katika kuhakikisha wizi huu wa kimtandao unadhibitiwa na
makampuni kuwa makini kuhakikisha yanalinda taarifa zake za siri.
No comments:
Post a Comment