Friday, July 1, 2016
ASKOFU WA KANISA KATHOLIKI JIMBO LA NJOME ALFRED MALUMA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KURIPOTI MATUKIO MAZURI NA SIYO MABAYA PEKEE
Muhashamu Askofu Wa Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Alfred Maluma Amevitaka Vyombo Vya Habari Nchini Kuacha Tabia Ya Kutoa Taarifa Za Maovu Pekee Na Badala Yake Vinapaswa Kufuatilia Taarifa Za Maendeleo Ya Wananchi Ikiwemo Tamaduni Zinazohamasisha Kuinua Uchumi Kwa Jamii .
Muhashamu Askofu Alfred Maluma Ametoa Rai Hiyo Akiwa Kwenye Makaburi Ya Mtaa Wa Mpechi Katika Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Wakati Akiongoza Misa Takatifu Ya Mazishi Ya Marehemu Anziwike Kuyava Ambaye Amefariki Dunia June Akiwa Anapatiwa Matibabu Katika Hospitali Ya Ilembula .
Aidha Muhashamu Askofu Maluma Amepongeza Utamaduni Wa Ushirikiano Uliopo Katika Jamii Wa Kusaidiana Katika Matatizo Mbalimbali Na Kuwataka Viongozi Wa Serikali Na Taasisi Za Kidini Kuendelea Kuhamasisha Wananchi Kudumisha Tamaduni Hizo Ili Kuleta Mabadiliko Ya Kiuchumi Katika Taifa Na Wananchi Husika.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Wananchi Wa Kata Ya Mjimwema Diwani Wa Kata Hiyo Abuu Mtamike Ametaka Wananchi Kumkumbuka Mungu Kila Siku Kwa Kuyakabidhi Maisha Yao Kwani Binadamu Hajui Siku Wala Saa Ya Kufariki Nakwamba Mwanadamu Duniani Ni Mpitaji.
Awali Akisoma Historia Ya Marehemu Anziwike Kuyava Kwa Niaba Ya Wanadugu Diwani Mstaafu Wa Kata Ya Mjimwema Jimmy Ngumbuke Amesema Marehemu Enzi Ya Uhai Wake Alikuwa Akisumbuliwa Na Ugonjwa Wa Moyo Na Mgongo Hadi Mauti Yanamkuta Alikuwa Akilalamika Kukosa Pumzi Na Hatiye Kufariki June 26 Mwaka Huu Akiwa Hospitali Ya Ilembula.
.............................................................................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment