Wasanii
wa Kikundi cha Butterfly Arts Group kilichokuwa kinafanya maonesho ya
sarakasi nchini India, Kulia ni kiongozi wa kikundi hicho Selemani
Pembe, Mwanaidi Abdallah, Abdallah Mkumba<hamidi Mbwana na Salem
Mbugio.
——————————————————–
Na Mwandishi wetu
KIKUNDI cha sarakasi cha Butterfly Arts Group kimerejea nchini juzi kutoka India kufanya maonesho ya sanaa ya sarakasi.
Katibu wa kikundi cha Butterfly
Arts Group, Selemani Pembe alisema jana Dar es Salaam kuwa katika ziara
yao ya kikazi nchini India iliyodumu kwa mwaka mmoja ilikuwa na
mafanikio makubwa ambapo wasanii wote sita wa kikundi hicho wamepata
mafunzo ya kutosha ya kufanya maonesho ya sarakasi.
Pembe ambaye pia ni mwalimu wa
Sarakasi nchini aliyewahi kuongoza vikundi vya sanaa vya DDC Kibisa,
Muungano Culture Troup, Makutano Dancing Troup, Ujamaa Ngoma Troup
alisema katika kipindi chote cha kuonesha sanaa ya sarakasi wamegundua
kuna utofauti mkubwa kati ya sanaa za maonesho za Tanzania na India.
Alisema wacheza sarakasi wa India
wanatumia vifaa vya kufunga juu ya jukwaa na kubembea juu kwa juu
tofauti na hapa nchini ambapo hakuna kumbi za kufunga vifaa maalum kwa
ajili ya kuonesha sarakasi hizo.
Pembe alisema pamoja na kasoro
hizo sarakasi ya Tanzania imekubalika sana nchini India hasa staili ya
kujenga maumbo (Pyramid, kujenga minara mbalimbali na kucheza ngoma za
asili.
Alisema maonesho mengine
yanayowavutia wanamichezo nchini India ni mchezo wa Limbo ambao
mwanasarakasi anapita katikati ya moto chini ya bomba maalum ambalo
limewashwa moto mkubwa na mchezo mwingine ni ule wa kupanda bomba kwa
staili mbalimbali mithili ya nyani.
Alisema katika kipindi cha mwaka
mmoja walikuwa wakifanya maonesho na Kampuni ya New Rambo Circus
inachofanya maonesho katika miji mbalimbali nchini India na nchi jirani.
Alisema wakiwa huko walifanya maonesho katika miji ya Pune, Bangalore, Gujirat, Mumbay na miji ya mipakani na nchi ya Nepal.
No comments:
Post a Comment