Ujumbe
wa wanaharakati wa maendeleo ya jinsia na watoto waliokutana na waziri
wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,wa kwanza kushoto ni
mkurugenzi wa TGNP Liliani Liundi,katikati ni Naemy Sillayo toka LHRC na
Janeth Mawinza kutoka WAJIKI
Picha
ya pamoja kati ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu pamoja na Wajumbe hao na viongozi wa
Wizara(Picha na Wizara ya Afya)
———————————————————-
———————————————————-
Na. Catherine Sungura. WAMJW
Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa dhamira ya kufikiwa kwa uwakilishi wa 50
kwa 50 katika ngazi mbalimbali za maamuzi inchini inafikiwa.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na ujumbe wa wanaharakati wa
maendeleo ya jinsia na watoto waliofika ofisini kwake na kufanya nao
mazungumzo
Mhe.Ummy
Mwalimu alisema jitihada zinafanyika kuhakikisha kuwa teuzi mbalimbali
zinahusisha jinsia zote, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa bodi mbalimbali
za uongozi wa Idara na Taasisi za Serikali.
“Nitoe
wito wangu kwa Mashirika mbalimbali ya Serikali na Yasiyo ya Serikali
kuzingatia usawa wa jinsia wakati wa teuzi mbalimbali za uongozi wa juu
pamoja na wajumbe wa Bodi”.
Aidha,
amewathibitishia wajumbe hao kuwa serikali ina dhamira ya dhati ya
kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Ndoa, “jitihada za maksudi
zinafanyika kuhakikisha marekebisho ya kifungu cha 13 na 17 cha sheria
ya ndoa, kinachoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa vinafanyiwa
marekebisho kwa kuwasilisha muswada Bungeni kabla ya mwaka kuisha.
Hata
hivyo alisema jitihada hizo za kufanya mabadiliko ya sheria zitahusisha
pia sheria ya Mirathi inayomnyima mtoto wa kike na wanawake kurithi
mali.
Akizungumza
kwa niaba ya ujumbe huo wa wanaharakati, mkurugenzi wa Mtandao wa
jinsia Tanzania (TGNP) bi. Liliani Liundi alisema ipo haja ya Serikali
kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha sheria ya Ndoa kifungu cha 13 na
17 inafanyiwa marekebisho, kwakuwa inarudisha nyuma jitihada za kuleta
usawa wa jinsia nchini.
Aidha,
alieleza kuwa mabadiliko ya Sheria ya Elimu katika kifungu
kinachokataza kuoa / kuoza mtoto wa shule ya Msingi na Sekondari ni
jitihada inayohitaji kuungwa mkono.
“Ipo
haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuwalinda watoto walio nje ya shule,
kwakuwa mabadiliko haya ya sheria ya Elimu yaliyopitishwa na Bunge la
11 yawewaacha nje pasipo ulinzi wa sheria watoto wengi walio nje ya
shule”Alisema.
Ujumbe
wa wanaharakati uliwasilisha maoni yao na changamoto mbalimbali zinazo
ikabili nchi katika kuleta maendeleo ya mtoto na usawa wa jinsia nchini,
ikiwa ni pamoja na suala la Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Nafasi ya
uwakilishi wa mwanamke katika vyombo mbalimbali vya maamuzi.
Ujumbe huo
uliongozwa na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bibi Lilian Liundi na
Wanaharakati wa Shirika la LHRC, WAJIKI, TANZANIA Widows Association na
shirika la Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAGIC)
No comments:
Post a Comment