Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, July 1, 2016

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa yaendelea na uhakiki wa Vyama Nchini.

Zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa kwa upande wa Tanzania Bara linaendelea .Tayari vyama 18 vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa kuhakikiwa Julai 4. Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu ambalo hufanyika kila mwaka ili kupima endapo vyama vya siasa vinakidhi matakwa ya Sheria ya usajili wa vyama vya Siasa.

Uhakiki wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo hugusa uhai wa kila chama cha siasa. Kwa upande wa Tanzania Visiwani , uhakiki unatarajiwa kuanza mara baada ya kumalizika Bara kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye.
Esther B.Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni Malapa Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na Mipango.(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa)
Msajili Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi. Piencia Kiurea akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party (UDP) Bw. Godluck Ole-Medeye wakati akitoa taarifa muhimu za chama chake katika zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Kisiasa unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Msajili Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi. Piencia Kiurea akikagua baadhi ya taarifa za Chama cha Mapinduzi “CCM” jana wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa uliofanyika katika Ofisi ndogo za chama hicho Jijini Dar es salaam
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Usajili wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kushoto) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha NRA ( National Reconstruction Alliance) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila (kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
 

Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini Buguruni Dar es salaam .
Bw.Eugene Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) akitoa taarifa wa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam leo
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki liliofanyika Leo katika ofisi za chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
 

No comments:

Post a Comment