Saturday, July 2, 2016
TAMASHA LA TUSEME LA JENGA UJASILI KWA WATOTO KUDAI HAKI ZAO SHULENI NA NYUMBANI KATIKA HALMASHAURI MBILI ZA NJOMBE
Baadhi Ya Wanafunzi Na Walimu Wa Shule Za Wilaya Ya Makete Na Njombe Wameelezea Mafanikio Mbalimbali Yaliyopatikana Tangu Kuanzishwa Kwa Mradi Wa Tuseme Ambao Unafadhiliwa Na Shirika La Unicef Kwamba Umesaidia Kuwapatia Ujasili Wa Kudai Haki Zao Watoto Wa Kike Wakiwa Shuleni Kwa Kuomba Kujengewa Vyumba Vya Kwaajili Ya Kubadilishia Nguo Na Kujisitili.
Wakizungumza Na Uplands Fm Mara Baada Ya Kumalizika Kwa Tamasha La Siku Moja Lililofanyikia Ukumbi Wa Kanisa Katholiki Nazareth Baadhi Ya Wanafunzi Wa Kutoka Shule Za Wilaya Ya Makete Na Njombe Wamesema Mradi Huo Wa Tuseme Umeongeza Uelewa Kwa Wanafunzi,Wazazi Na Walimu Ambao Wamehimiza Serikali Na Wafadhili Kujenga Vyumba Kwaajili Ya Watoto Wa Kike Sheleni.
Aidha Wanafunzi Hao Wameshukuru Kuanzishwa Kwa Klabu Za Wanafunzi Katika Shule Hizo Kwa Lengo La Kukabiliana Na Changamoto Zinazowakabili Watoto Wa Kike Wakiwa Shuleni Huku Wakishukuru Kuanzishwa Kwa Klabu Katika Shule Ili Waweze Kudai Haki Zao Wakiwa Nyumbani Na Shuleni Na Kuwataka Watoto Wengine Kujiunga Na Klabu Hizo Kwa Manufaa Yao.
Valian Ngalioma Ni Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Ninga Na Mwalimu Hekima Luvanda Magoye Wamesema Kuanzishwa Kwa Klabu Za Tuseme Kwa Wanafunzi Shuleni Kumesaidia Watoto Kudai Haki Zao Kwa Wazazi Na Walezi ,Shuleni Wametengewa Vyoo Bora Na Vyumba Vya Kujisitili Watoto Wa Kike Na Kusaidia Kuongeza Kiwango Cha Ufaulu Kwa Wasichana Wa Shule Za Msingi.
Akizungumza Kwenye Tamasha Hilo La Tuseme Kwa Niaba Ya Afisa Elimu Mkoa Wa Njombe,Mratibu Wa Shughuli Za UNICEF Mkoa Pamoja Na Wawakilishi Wa UNICEF Wilaya Za Makete Na Njombe Akiwemo Sifa Mfaramagoha Wamesema Wamefanikiwa Kuzifikia Shule Mbalimbali Za Wilaya Zao Ili Kufungua Klabu Hizo Kwa Lengo La Kuwasaidia Watoto Kudai Haki Zao.
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Kupitia Kitengo Cha Dawati La Jinsia Nalo Likatumia Fursa Hiyo Kuwataka Wananchi Hususa Wazazi Na Walezi Pamoja Na Walimu Kuacha Tabia Za Unyanyasaji Na Ukatili Kwa Watoto Hao Huku Watoto Nao Wakitakiwa Kuondoa Hofu Za Kuwataja Walimu Na Wazazi Na Walezi Wanaowafanyia Vitendo Vya Ukatili Ili Hatua Za Kisheria Zichukuliwe Dhidi Yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment