Saturday, July 2, 2016
APEC YATOA ELIMU YA UDEREVA KWA WAMILIKI NA MADEREVA WA PIKIPIKI MAARUFU BODABODA MAKAMBAKO
Jumla Ya Madereva Wa Pikipiki 300 Wa Halmashauri Ya Mji Wa Makambako Wamefanikiwa Kuhitimu Mafunzo Ya Udereva Ambayo Yametolewa Na Jeshi La Polisi Kwa Kushirikiana Na Shirika Lisiro La Kiserikali La Kupunguza Umasikini Na Kutunza Mazingira APEC Yalitolewa Kwa Kipindi Cha Siku Sita Katika Vituo Mbalimbali Vya Halmashauri Hiyo.
Akifunga Mafunzo Ya Udereva Kwa Niaba Ya Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Pudensiana Plotas ,Kaimu Kamanda Wa Jeshi Hilo SSP Nicodemus Katembo Amepongeza Kwa Muamko Mkubwa Ulioonekana Kwaajili Ya Kupatiwa Mafunzo Ya Udereva Na Kusema Kuwa Matukio Ya Ajali Yatapungua Endapo Madereva Watatumia Elimu Hiyo Kufuata Sheria Na Kanuni Za Usalama Wa Barabarani.
Aidha Kaimu Kamanda Katembo Amesema Madereva Wa Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Wanatakiwa Kuwa Makini Na Abiria Wanaowasafirisha Kwa Kuimarisha Ulinzi Shilikishi Kwa Kutumia Mbinu Walizofundishwa Kwenye Mafunzo Hayo Za Polisi Jamii Katika Kuwafichua Wharifu Ambao Wanania Ya Kwenda Kufanya Tukio La Uharifu Kwani Wengi Wao Wanatumia Usafiri Wa Pikipiki Ambao Wa Haraka.
Katembo Amesema Pamoja Na Kwamba Madereva Hao Wamefanikiwa Kupewa Vyeti Vya Kuhitimu Mafunzo Hayo Lakini Wanatakiwa Kwenda Kuchukua TIN. Namba Inayotolewa Na Ofisi Ya TRA Mkoa Wa Njombe Bure Na Hatimaye Kwenda Kufuata Leseni Za Udereva Mkoani Luvuma Tayari Kwa Kuendelea Na Kazi Za Udereva Pasipo Kupewa Usubufu Wowote.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika Lisilo La Kiserikali La Kupunguza Umasikini Na Kutunza Mazingira APEC Respicius Timanywa Amebainisha Baadhi Ya Vituo Ambavyo Wameshiriki Kutoa Mafunzo Hayo Kuwa Ni Pamoja Na Mlowa,Kitandililo,Ilunda, Makambako Mjini Na Manga Ambapo Amesema Mafunzo Hayo Bado Yanaendelea Kwa Baadhi Ya Maeneo Katika Halmashauri Hiyo.
Awali Akisoma Tarifa Ya Kufunga Mafunzo Hayo Kwa Niaba Ya Madereva Wote Said Jokoro Amepongeza Shirika Lisilo La Kiserikali La Kupunguza Umasikini Na Kutunza Mazingira APEC Kwa Jitihada Wanazofanya Za Kuwawezesha Madereva Hao Kupata MafunzoYa Udereva Pamoja Na Jeshi La Polisi Huku Ombi Lao Ni Kuwekewa Vituo Maalumu Kwaajili Ya Kupaki Ili Wawe Marafiki Na Askali Wa Barabarani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment