Saturday, July 2, 2016
MILA POTOFU ZINAZOHATARISHA USALAMA WA WALEMAVU WA NGOZI NA WALEMAVU WA VIUNGO ZA PIGWA VITA NJOMBE
Wananchi Wilayani Njombe Wametakiwa Kushirikiana Na Viongozi Wao Kupambana Na Ukatili Wa Kijinsia Dhidi Ya Watoto Na Akina Mama Kwa Kuondoa Mila Potofu Na Kandamizi Katika Jamii Ambazo Zimeonekana Kuwakandamiza Akina Mama Na Watoto Wao Ili Haki Itendeke Pande Zote Miongoni Mwa Familia.
Rai Hiyo Imetolewa Na Afisa Ustawi Wa Jamii Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Julitha Kazimiri Wakati Akizungumza Na Wananchi Wa Vijiji Vya Iwafi Na Lwanzari Kwenye Midahalo Ya Kuelimisha Wananchi Kuzuia Na Kupambana Na Mila Potofu Ambazo Ni Kandamizi Zinazosababisha Kuwepo Kwa Ukatili Wa Kijinsia Kwa Watoto Na Akina Mama.
Bi.Kazimiri Amesema Wazazi Na Walezi Wanatakiwa Kutoa Adhabu Zinazostahili Kwa Watoto Wao Siyo Kuwapiga Hadi Kuwaumiza Nakwamba Idadi Kubwa Ya Akina Baba Ndiyo Wanaoongoza Kuwatelekeza Wake Na Watoto Ambao Wamekuwa Wakikabiliwa Na Jukumu La Kuwalea Bila Baba Zao Kushiriki Kusaidia Mahitaji Ya Msingi Ikiwemo Kuwapatia Haki Ya Msingi Ya Elimu.
Akitoa Mada Mwezeshaji Wa Midahalo Hiyo Ambaye Pia Ni Afisa Ustawi Wa Jamii Wilaya Herieth Magaji Amesema Ukatili Wa Kijinsia Katika Jamii Si Kupigwa Pekee Bali Hata Mila Zinazoendekezwa Na Baadhi Ya Jamii Zikiwemo Za Ukeketaji,Ubakaji Unaofanywa Na Baadhi Ya Wazazi Kufanya Mahusiano Ya Kimapenzi Na Watoto Wao Ambapo Hali Hiyo Ina Sababishwa Na Baadhi Ya Waganga Wa Jadi Wenye Mila Potofu.
Awali Wakichangia Mada Kwenye Midahalo Ya Kupinga Ukatili Wa Kijinsia Dhidi Ya Watoto Na Akina Mama Baadhi Ya Wananchi Wamekili Kuwepo Kwa Mila Potofu Ambazo Zinawakandamiza Watoto Na Akina Mama Zikiwemo Za Kuwatenga Walemavu Na Kuwa Na Mitara Katika Ndoa Jambo Ambalo Linasababisha Kuwakosesha Watoto Haki Za Msingi Za Elimu Na Malezi.
Leo Midahalo Hiyo Inayoendeshwa Na Ofisi Ya Ustawi Wa Jamii Wilaya Ya Njombe Inatarajia Kuendelea Katika Vijiji Vya Nyave Na Ikondo Kwaajili Ya Kuhamasisha Wananchi Kukemea Ukatili Wa Kijinsia Na Kutowatenga Watu Wenye Ulemavu Wa Viungo Mbalimbali Waliopo Katika Maeneo Yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment