Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, July 19, 2016

SHULE YA MSINGI SOVI KATA YA MTWANGO WILAYANI NJOMBE YATARAJIA KUFANYA HARAMBEE YA KUCHANGIA UKARABATI WA VYUMBA VYA MADARASA NA NYUMBA ZA WALIMU

 Hawa Ni Wajumbe Wa Kamati Ya Shule Na Harambee  Ya Uchangiaji  Ukarabati Wa Madarasa  Na Nyumba Za Walimu


 Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Sovi Ezekiel  Chaula Wa Upande Wa Kulia Na Wa Kushoto Ni Mkurugenzi Wa Taasisi Ya Mafanikio Foundation Michael Uhahula


 Madawati Nayo Yanawasubiria Kulipa Deni La Shilingi Milioni Mbili Zinazotegemea Michango Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Sovi Na Mwango Wanaosoma Kwenye Shule Hiyo

Mwenyekiti Wa Kamati Ya Shule Hance Luwanja Akizungumza Na Wajumbe Kuhusiana Na Maandalizi Ya Harambee Ya Kuchangia Ukarabati Wa Vyumba Vya Madarasa Na Nyumba Za Walimu  Katika Shule Ya Msingi Sovi Wilayani Njombe.

Wanachi Na Wadau Wa Elimu Mkoani Njombe Wameombwa Kujitokeza Kuchangia Ukarabati Wa Miundombinu Ya Shule Ya Msingi Sovi Kata Ya Mtwango Wilayani Njombe Ambayo Inakabiliwa Na Uchakavu Wa Madarasa Na Nyumba Za Walimu  Kwa Lengo La Kuboresha Mazingira Hayo Yaweze Kuvutia Utendaji Kazi Na Kujisomea Kwa Wananchi Wa Shule Hiyo.

Rai Hiyo Imetolewa Na Mwenyekiti Wa Kamati Ya Shule Ya Msingi Sovi Hance Luwanja Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na  Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili Wananchi Wa Kijiji Cha Sovi  Na Kusema Kuwa Tatizo Kubwa Ni Uchakavu Wa Madarasa Ya Shule Na Nyumba Za Walimu Ambazo Haziwahi Kukarabatiwa  Tangu Zijengwe Miaka 30 Iliyopita.

Aidha Luwanja Amesema Kutokana Na Uchakavu Huo Kamati Ya Shule Kwa Kushirikiana Na  Serikali Ya Kijiji  Wamelazimika Kuandaa Mkutano  Na Kuwaalika Wadau Wa Elimu Wa Kutokana Maeneo Mbalimbali Ya Mkoa Wa Njombe Akiwemo Mbunge Wa Jimbo Hilo Joram Hongori ,Taasisi Na Makampuni  Kwa Lengo La  Kusaidia Uchangiaji  Ujenzi Huo  Kwenye Harambee Itakayofanyika  Augost 27 Mwaka Huu.

Akizungumza Kwa Upande Wake Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Sovi Ezekia Chaula  Amesema Kuwa Shule Hiyo  Licha Ya Kuchakaa Kwa Madarasa Lakini Pia Milango Nayo Ni  Chakavu  ,Nyumba Za Walimu Zinakatisha  Nia Ya Kuendelea Kufundisha  Wanafunzi Hususani  Msimu Wa Mvua  Ambao Walimu Hulazimika Kuacha Masomo Kwenda Kuhifadhi  Mali Nyumbani Zisivujiwe Na Maji Ya Mvua.

Mkurugenzi Wa Taasisi Ya Mafaniko Foundation  Michael Uhahula  Amewahimiza Wadau Wengine Na Wazazi  Kujenga Moyo Wa Kujitolea Kuboresha Mazingira Ya Elimu  Kwa Manufaa Ya  Wanafunzi  Ambapo Jitihada Za Ukarabati Huo Zinatakiwa Zienze Na Wakazi Wa Kijiji Hicho Ndipo Wadau  Nao Washiriki  Na Kwamba Taasisi  Hiyo Imeahidi  Kudhamini Tukio La Harambee Ili Kufanikisha Harambee Hiyo.

Noel Ndunduru Ni Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Sovi Amesema Serikali Na Wananchi Wake Wameunga Mkono Jitihada Za Kamati Ya Shule  Kufanya Harambee Ili Kufanikisha Kupatikana  Kwa Fedha Zaidi Ya Shilingi Milioni  20  Kwaajili Ya Kuboresha Mazingira Ya Shule Kwa Kukarabati Madarasa Na Nyumba Za Walimu Ambazo Zimechakaa.

No comments:

Post a Comment