Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, July 18, 2016

KUTOA MSAADA HAIMAANISHI NI KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUKWEPA KODI-MAKONDA


.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati)akipokea moja ya bati  kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Subash Patel ikiwa ni sehemu msaada wa kupaulia vyumba madarasa leo jijini Dar es Salaa , Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa, Thelesia Mmbando. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiangalia mtambo wa kutibu maji taka na kuweza kutumika katika matumizi mengine wakati alipotembelea matambo huo katika kiwanda cha uzalishaji bati cha MMI Steel. 

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa wanaotoa misaada haimaanishi kuwa wanataka kutengeneza mazingira  ya kukwepa kodi,ni wajibu wa kampuni au taasisi kuguswa kwa namna moja ama nyingine katika kusaidia kutatua changamoto zinazoizunguka jamii .

Makonda ameyasema hayo leo,wakati wa makabidhiano wa bati 10000,na madawati 1000, kutoka kwa kampuni ya kuzalisha bati ya MMI Steel na Baps Charity amesema kuwa kampuni hiyo imefungua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Makonda amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli alitoa bilioni mbili hivyo bati hizo zitakwenda katika kupaua vyumba vya madarasa na bati zingine zitabaki hivyo wadau waitikie wito wa kujenga vyumba vya madarasa.

Amesema kampuni hiyo imetoa sehemu yake katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Pombe Magufuli ya elimu bure ambayo itaendana na mazingira bora ya kusomea.

Makonda amesema kuwa kampuni hiyo imeweka mtambo wa majitaka kusafisha na kutumika tena na kutaka kampuni zingine zifanye hivyo.
Amesema kuwa wenye viwanda kuacha kutumia mitaro ya mvua kutiririsha maji na kutengeneza mifumo yao.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Subash Patel amesema kuwa wameona umuhimu wa elimu na jitihada za Rais na kuamua kutoa sehemiu ya uwezo wao.Patel amesema kuwa wataendelea kutoa kadrichangamoto zinapoibuka.

No comments:

Post a Comment