Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, July 19, 2016

MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKABIDHI ZAWADI ZA USHINDI WA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA KWA WASHINDI


 KULIA NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI ,KATIKAKTI NI MBUNG E WA JIMBO LA LUPEMBE JORAM HONGORI NA WA TATU KUTOKA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI


 HAPA MKUU WA MKOA WA NJOMBE ANAKABIDHI ZAWATI ZA USHINDI WA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA AMBAZO NI PIKIPIKI NA GARI KWA VIJIJI NA HALMASHAURI


 PICHA YA PAMOJA NA  VIONGOZI WA KIJIJI CHA WANGINYI MWENYEKITI EMMANUEL MWENDA AKIWA NA MTENDAJI WA KIJIJI CHAKE WALIOCHUCHUMAA NA KUSHIKA KIKOMBE NA HATI WAKIWA NA VIONGOZI WA MKOA WAKIONGOZWA NA MKUU WA MKOA REHEMA NCHIMBI.
 ZAWADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE NA HAWA NI WATALAAMU WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA



Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amewataka Watalaamu Wa Halmashauri Na Wananchi  Kuhakikisha Wanasimamia Kikamilifu Dhana Ya Afya Na Usafi Wa Mazingira Kwa Kujenga Vyoo Bora Vya Kisasa  Kwaajili Ya Kuzuia Mlipuko Wa Ugonjwa Wa Kipindupindu  Ambapo Amewaagiza Madiwani Wa Halmashauri Zilizopo Kuweka Agenda Ya Kwanza Ya  Kampeni Ya Ujenzi Wa Vyoo Kwenye Vikao Vyao.

Kauli Hiyo Ameitoa Mkuu Wa Mkoa Wa  Njombe Dkt Rehema Nchimbi Wakati Akikabidhi Na Kupongeza  Baadhi Ya Halmashauri Zilizofanya Vizuri Kwenye Mashindano Ya Kampeni Ya Afya Na Usafi Wa Mazingira  Ambayo Wilaya Ya Njombe Imeibuka Mshindi Wa Kwanza Kitaifa Na Kuzawadiwa Zawadi Ya Gari Aina Ya Land Cruzer Huku Vijiji Vyake Vya Halmashauri Hiyo Vikizawadiwa Pikipiki Na Makombe.

Aidha Dkt Nchimbi Amesema  Kuna Baadhi Ya Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Ambazo Hazikufanikiwa Kupata Ushindi Vyoo Vyake  Siyo Vya Kisasa Na Hivyo Kutaka Kwenda Kuboresha  Kuliko Kusubilia Ushindi Ndipo Watekeleza Dhana Ya Ujenzi Wa Vyoo Bora Vya Kisasa  Huku Akizuia   Misaada   Ya Kujengewa Vyoo Vya Kisasa Badala Yake  Viongozi Wa Vijiji,Kata Na Halmashauri Wajenge Wenyewe Kwa Nguvu Zao.

Awali Akimkaribisha Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi,Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Luth  Msafiri Amepongeza Kwa Mshikamano Uliooneshwa   Wa Viongozi Na Wananchi Kufanikisha Kupata Ushindi  Na Tuzo Hizo Na Kutaka Kwenda Kulifanyia Kazi Tatizo La Kukosekana Kwa Huduma Za Maji Ya Bomba Kwa Baadhi Ya Vijiji Na Mitaa.

Kwa Upande Wake Baadhi Ya Viongozi Wa Vijiji Mbalimbali Vilivyopatiwa Ushindi Wa Usafi  Na Usafi Wa Mazingira Ikiwemo Kijiji Cha Wanginyi,Matiganjora Na Sovi Kata Ya Mtwango Wilayani Njombe Wakizungumza Kwa Niaba Ya Wananchi Wao Wamepongeza Halmashauri Kwa Kuwapatia Mashindano Hayo  Na Kuahidi Kwenda Kutekeleza Zaidi Ili Kila Mwaka Vijiji Hivyo Viwe Vinashinda.

No comments:

Post a Comment