Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. Jakaya Kikwete akiwahutubia
wajumbe wa mkutano mkuu Maalum kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre
mjini Dodoma, ambapo mkutano huo utamthibitisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli aliyekaa kulia kuwa
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa akipokea uongozi huo kutoka kwa mtangulizi
wake Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa
Chama cha mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete, Wajumbe wengi wamehudhuria
katika mkutano huo wanatarajia kupiga kura hiyo muda wowote kuanzia sasa
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi Bara , Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
na wa pili kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali
Mohamed Shein.
PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa
maelezombalimbali na kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama Dk Jakaya
Kikwete katika Mkutano Mkuu Maalum ili kuufungua tayari kwa
kumthibitisha
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti mtarajiwa wa CCM Dk.
John Pombe magufuli wa pili kutoka kushoto akishiriki kuimba wimbo wa
taifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM anayeng’atuka madarakani Dk. Jakaya
Kikwete wa pili kulia wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar wa
tatu kutoka kushoto, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM taifa Mzee Benjamin
William Mkapa na kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Ali Hassan Mwinyi akishiriki kuimba nyimbo kabla wakati wa mkutano huo.
Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar SMZ Mhe. Mohammed Said Mohammed Dimwa
Mama
Salma Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka mkoa wa Lindi
akishiriki kuimba nyimbo za hamasa na pamoja nawake wa viongozi wenzake.
Mwenyekiti
wa Chama cha Tanzania Labour Part TLP Bw. Agustino Lyatonga mrema na
viongozi wenzake wa vyama vilivyoalikwa katika mkutano mkuu Maalum wa
CCM unaofanyika mjini Dodoma
Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar SMZ Mhe.
Mohammed Said Mohammed Dimwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakishiriki kuimba nyimbo za hamasa.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kushoto na Mzee Said El Maamry na wageni waalikwa wengine wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Anthony Dialo akiwa na wajumbe wenzake
kutoka mkoani Mwanza wakiwa katika mkutano huo, Kulia ni Richard Ndasa
na wa tatu ni Ndugu John Mongela.
Baadhi ya wajumbe kutoka mkoa wa Iringa kutoka kulia ni Dk Agustine Mahiga na Salim Abri Asas pamoja na wenzao wakiwa katika mkutano huo.Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma uliomalizika saa mbili zilizopita.
Baadhi ya wake wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo
Baadhi ya viongozi wastaafu
wakipitia gazeti la uhuru lenye makala maalumu ya Dk. John Pombe
Magufuli anayetarajiwa kuthibitishwa leo kuwa Mwenyekiti wa Cma cha
Mapinduzi CCM.
Wajumbe kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe kutoka mkoa wa Morogoro nao hawakuwa nyuma kupitia makala ya Gazeti la Uhuru leo.
Mwimbaji wa kundi la Hamasa la CCM TOT Bi. Khadija Kopa na waimbaji wenzake wakitumbuiza katika mkutano huo.
Mmoja wa waalikwa akipata kumbukumbu katika mkutano huo.
Kundi la Hamasa la TOT likiendelea na burudani katika mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wakiongozwa na
Mjumbe Angela Kairuki kutoka mkoa wa Dar es salaam wakiserebuka kabla ya
kuanza kwa mkutano huo.
Dk. Fenella Mukangara kutoka mkoa wa Dar es salaam na Tambwe Munde kutoka mkoa wa tabora wakiserebeka pamoja na wajumbe wenzao.
Mjumbe Munde Tambwe akisalimiana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba.
Mjumbe Fredrick Mwakalebela kutoka mkoa wa Iringa akiwa na wajumbe wenzake.
TOT ikiendelea kutumbuiza
Mwakipesile na Mary Mwanjelwa Wajumbe kutoka mkoani Mbeya wakisalimiana kwa furaha.
No comments:
Post a Comment