Thursday, May 12, 2016
WAUGUZI WA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE WAITAKA SERIKALI KULIPA FEDHA ZA LIKIZO KABLA YA KWENDA LIKIZO
WAUGUZI WAKIWA KWENYE MAANDAMANO KUTOKEA HOSPITALI YA TANWAT KUELEKEA CHUO CHA WAUGUZI KIBENA
MGENI RASMI KATIBU TAWALA MSAIDIZI GIDEON MWINAMI AKIPOKEA MAANDAMANO HAYO
WAUGUZI WANAWASHA MISHUMAA YA ISHARA YA UPENDO
MGENI RASMI BAADA YA KUSIMAMA KUTOA HOTUBA YAKE
WAUGUZI WAKIPELEKA ZAWADI KWA WAUGUZI WANAOTARAJIA KUSTAAFU
RISALA YA WAUGUZI IKIWASILISHWA KWA MGENI RASMI LEO KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA WAUGUZI KIBENA
WAUGUZI HAPA WANAONESHA FANI YA KUIGIZA KWA NKUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA WAKIWA MBELE YA MGENI RASMI
HUU NDIYO UKUMBI WA CHUO CHA UUGUZI KIBENA
Zaidi Ya Wauguzi 200 Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Leo Wameungana Na Wauguzi Wengine
Kuadhimisha Siku Ya Wauguzi Duniani Kote Ambapo Katika Kuadhimisha Siku Hiyo Wamefanikiwa
Kufikisha Changamoto Mbalimbali Ambazo Zimekuwa Zikiwakabili Wauguzi Wakati Wa Kutekelez
Majukumu Yao Ikiwemo Kutopatiwa Mafao Ya Kustaafu Kutoka Mashirika Ya Hifadhi Ya Taifa Ya Jamii.
Akizungumza Kwenye Maadhimisho Hayo Kwa Niaba Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Jackson
Saitabahu,Katibu Tawala Msaidizi Gideon Mwinami Ametaka Wauguzi Kuitumia Siku Hiyo Kwaajili Ya
Kukumbushana Utekelezaji Wa Majukumu Yao Kwa Uadilifu Na Kufuata Misingi Ya Maadili Ya Utendaji
Kazi Kwenye Vituo Vyao.
Kuhusu Malalamiko Ya Wauguzi Kutopandishwa Vyeo Na Kuongezewa Mishahara Pindi Wanapotoka
Masomoni Katibu Msaidizi Huyo Mwinami Ameahidi Kuzifikisha Changamoto Hizo Kwa Mkurugenzi Wa
Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ili Kutatua Zile Zilizo Chini Ya Uwezo Wake Huku Akitaka Jamii
Kuwathamini Wauguzi Hao Kwa Kuonesha Ushirikiano Wakati Wa Kutekeleza Majukumu Yao.
Rustika Mtemba Ni Mwenyekiti Wa Chama Cha Wauguzi Halmashauri Ya Mji Wa Njombe TANNA
Ambaye Ametaka Serikali Kuwafikilia Swala La Kuwafanyia Mabadiliko Ya Kupandishwa Vyeo Na
Mishahara Wauguzi Wanapotoka Masomoni Huku Akitupia Lawama Mifuko Ya Taifa Ya Hifadhi Ya Jamii
Ikiwemo NSSF Kwa Kushindwa Kutoa Mafao Yao Kwa Wakati.
Katika Risala Ya Wauguzi Kwa Mgeni Rasmi Iliyosomwa Na Dativa Mwinuka Imeeleza Kuwepo Kwa
Changamoto Ya Wauguzi Kutopewa Sale Za Kazi,Kutolipwa Fedha Za Likizo Kwa Wakati,Fedha Za Masaa Ya
Ziada Ambapo Wamefanikiwa Kupunguza Vifo Vya Watoto Wachanga Na Watoto Chini Ya Miaka Mitano.
Kwa Upande Wao Wauguzi Wakizungumza Mara Baada Ya Hotuba Ya Mgeni Rasmi Wametaka Serikali Kuwaboreshea Mazingira Ya Kufanyia Kazi Kwaajili Ya Usalama Wao Ambapo Wametolea Mfano Hospitali Ya Kibena Ambayo Mazingira Yake Yanahatarisha Usalaama Wao Kwa Kukosa Uzio Na Kutaka Kupewa Malipo Ya Masaa Ya Ziada Pamoja Na Malipo Ya Likizo Yatolewe Kabla Ya Kwenda Likizo.
Maadhimisho Ya Siku Ya Wauguzi Duniani Kwa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Yamefanyikia Katika
Hospitali Ya Kibena Huku Kwa Mkoa Wa Njombe Yakifanyikia Wilayani Makete Yakiwa Na Kauli Mbiu
Isemayo Wauguzi Ni Nguvu Ya Mabadiliko Ya Uboreshaji Wa Mifumo Ya Afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment