Friday, May 13, 2016
BAADHI YA WANANCHI WA VIJIJI VYA MWILAVILA NA TAMBALANG'OMBE KATA YA MALANGALI WILAYA YA MUFINDI WALALAMIKIA KULAZIMISHWA KUWASHONEA WATOTO WAO FULANA ZENYE RANGI YA CCM
Serikali Wilayani Mufindi Mkoani Iringa Imepiga Marufuku Kuanzishwa Kwa Michango Na Sale Za Shule Ambazo Haziridhiwa Na Wananchi Ili Kuepusha Migogoro Isiyo Ya Lazima Baina Ya Walimu Na Wazazi Na Kutaka Walimu Wote Wa Shule Za Sekondari Na Msingi Kutojihusisha Na Kushika Fedha Za Michango Yoyote Ya Wananchi Kwenye Shule Zao.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Afisa Habari Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Mufindi Ndimmyake Mwakapiso Kufuatia Kuwepo Kwa Malalamiko Kutoka Kwa Wananchi Wa Vijiji Vya Mwilavila Na Tambalang'ombe Kulalamikia Uongozi Wa Shule Ya Msingi Ihanga Kuwalazimisha Kushona Fulana Za Wanafunzi Zenye Rangi Zinazofanana Na Za Chama Cha Mapinduzi.
Aidha Afisa Habari Huyo Bwana Mwakapiso Amemuagiza Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Ihanga Kata Ya Malangali Jacob Sanandala Kuacha Mpango Huo Wa Kulazimisha Wazazi Kuwashonea Watoto Wao Fulana Hizo Ikiwa Wazazi Hawajaridhia Huku Akitaka Walimu Wote Kufuata Miongozi Ya Elimu Waliyopewa Na Kusimamia Taaluma Shuleni.
Mwakapiso Amesema Michango Yote Itakayoanzishwa Kwenye Shule Ni Lazima Ilidhiwe Na Wazazi Na Kutaka Walimu Wakuu Wote Wawe Makini Katika Kipindi Hiki Ambacho Rais Magufuri Amepiga Marufuku Michango Yote Shuleni Huku Akikili Kupata Taarifa Za Kuanzishwa Mpango Wa Fulana Hizo Mbele Ya Mkutano Ambao Baadhi Ya Wazazi Hawakuridhia Na Kusema Sale Zinazotakiwa Ni Zile Zilizokuwa Zinatumika Zamani .
Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Ihanga Kata Ya Malangali Jacob Sanandala Ambaye Amesema Anayeweza Kulizungumzia Tatizo La Kulazimisha Wazazi Kuwashonea Fulana Wanafunzi Wa Shule Hiyo Ni Halmashauri Ya Wilaya Ya Mufindi Kwani Yeye Hana Mamlaka Yoyote Kulizungumzia Tatizo Hilo.
Awali Wananchi Wa Vijiji Vya Mwilavila Na Tambalang'ombe Wamelalamikia Uongozi Wa Shule Ya Msingi Ihanga Ukiongozwa Na Mwalimu Mkuu Wa Shule Hiyo Jacob Sanandala Kwa Kuwarudisha Nyumbani Watoto Kwa Kukosa Fulana Zenye Rangi Inayofanana Na Zile Za CCM Licha Ya Kutoridhia Mpango Huo MpyaWa Kuanzisha Fulana Hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment