MADEREVA WA BODABODA WA KATA YA UTARINGORO WAKIWA KWENYE MAANDAMANO WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO HAYO
WA UPANDE WA KULIA NI AFISA MFAWIDHI WA SUMATRA MKOA WA NJOMBE JOSEPH BURONGO,WA PILI KUTOKA KULIA NI MRATIBU WA FUTURE WORLD VOCATION CENTRE KUTOKA DAR ES SALAAM YUSTO WALISIMBA MKOLA NA WA TATU NI AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA UTARINGORO ISABELA MALANGALILA NAYE MIONGONI MWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA.
AFISA USALAAMA WA BARABARANI MKOA WA NJOMBE SANJENT BRAISON KAMBO AKITOA ELIMU JUU YA MAFUNZO WALIOPEWA MADEREVA HAO NA SHERIA ZAKE
AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA UTARINGORO ISABELA MALANGALILA AKISOMA LISARA YA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA AKIWEMO YEYE MWENYEWE NAYE KAPATIWA MAFUNZO HAYO
AFISA MFAWIDHI WA SUMATRA MKOA WA NJOMBE JOSEPH BURONGO AKIZUNGUMZA NA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA UTARINGORO
Serikali Mkoani Njombe Imewataka Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kuwa Wavumilivu Wakati Juhudi Za Kusogeza Huduma Mbalimbali Zikifanyika Ikiwemo Zoezi La Kutoa Leseni Kwa Waliopatiwa Mafunzo Ya Udereva Ambapo Ifikapo Mwezi Julai Mwaka Huu Leseni Za Udereva Zitakuwa Zinatolewa Mkoani Njombe.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Afisa Mfawidhi Wa Mamlaka Ya Udhibiti Wa Usafiri Wa Nchi Kavu Na Majini Mkoa Wa Njombe Sumatra Joseph Burongo Wakati Akifunga Mafunzo Ya Udereva Kwa Wahitimu Wa Mafunzo Hayo Katika Kijiji Cha Utaringoro Yaliyodumu Kwa Takribani Siku Saba Yakitolewa Na Wakufunzi Wa Kutoka Future World Vocation Centre Kutoka Jijini Dar Es Salaamu.
Burongo Amesema Mpango Wa Serikali Mkoa Wa Njombe Ni Kusogeza Huduma Karibu Na Wananchi Ambapo Kwa Upande Wa Madereva Wataendelea Kufuatilia Leseni Hizo Kwenye Mikoa Ya Luvuma,Mbeya Na Iringa Ambapo Amesema Kwa Wamiliki Wa Pikipiki Na Pikipiki Za Magurudumu Matatu Maarufu Bajaji Leseni Za Sumatra Wanachukulia Halmashauri Na Miji Husika.
Awali Akizungumza Afisa Usalaama Wa Barabarani Mkoa Wa Njombe Sajent Braison Kambo Ametaka Wahitimu Wa Mafunzo Hayo Wanatakiwa Kuzingatia Elimu Waliyoipata Kutoka Kwa Wakufunzi Hao Kwa Kwa Kuepukana Na Matukio Ya Ajali Huku Akitaka Kushawishi Madereva Wengine Wasiyo Na Leseni Wakiwemo Akina Mama Ili Kupunguza Vifo Vitokanavyo Na Ajali Za Barabarani.
Mratibu Wa Taasisi Ya Future World Vocation Trainning Centre Kutoka Jijini Dar Es Salaamu Yusto Walisimba Mkola Ametaka Wahitimu Hao Kulipia Bima Za Pikipiki Na Vyombo Vyao Vya Moto Kwa Manufaa Yao Huku Akisema Leseni Haiwezi Kuzuia Ajali Isipokuwa Ni Umakini Na Kuzingatia Alama Za Barabarani Ambacho Wamesisitiza Wakati Wa Utoaji Wa Mafunzo.
Isabela Malangalila Ni Miongoni Mwa Wahitimu Wa Mafunzo Hayo Akisoma Taarifa Fupi Kwa Niaba Ya Wahitimu Wote Ametaja Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili Madereva Wa Vyombo Vya Moto Zikiwemo Za Kufuata Leseni Na Huduma Nyingine Kutoka Nje Ya Mkoa Wa Njombe.
Kwa Upande Wake Wahitimu Wa Mafunzo Hayo Wamepongeza Taasisi Ya The Future World Vocation Centre Kwa Kuwapatia Mafunzo Hayo Na Kuelezea Namna Watakavyo Nufaika Kwani Wameahidi Kuitumia Elimu Waliyo Ipata Ipasavyo Na Kuwashawishi Madereva Wengine Kujiunga Na Mafunzo Ili Kuepukana Na Usumbufu Wa Kusimamishwa Na Kutozwa Faini Na Maafisa Usalaama Wa Barabarani.
No comments:
Post a Comment