JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
• WATU
WATATU WAMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA MASHOKA NA MWINGINE MMOJA
KUJERUHIWA KICHWANI WAKATI WAKIFANYA IBADA KATIKA MSIKITI WA MASJID
RAHMANI ULIOPO ENEO LA IBANDA RELINI WILAYANI NYAMAGANA.
MNAMO
TAREHE 18.05.2016 MAJIRA YA SAA 20:30HRS KATIKA MSIKITI WA MASJID RAHMAN
ULIOPO IBANDA RELINI MTAA WA UTEMINI @ MAPANKINI KATA YA MKOLANI WILAYA
YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA.
WATU WASIOZIDI 15 WAKIWA WAMEVALIA
MAVAZI YA KUFICHA USO WAKIWA NA MAPANGA, SHOKA NA BENDERA NYEUSI YENYE
MAANDISHI MEUPE WALIINGIA GHAFLA KATIKA MSIKITI TAJWA HAPO JUU WAKATI
WAUMINI WA MSIKITI HUO WAKIWA WANASWALI NA KUZIMA TAA NA KUTOA SAUTI
WAKISEMA “KWA NINI MNASWALI WAKATI WENZETU WAMEKAMATWA NA WANASHIKILIWA
NA POLISI ?” NA HAPO HAPO WAKAANZA KUWAKATA KWA MAPANGA BAADHI YA
WAUMINI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO.
WALIPATA MAJERAHA MAKUBWA
KICHWANI, SHINGONI NA MIKONONI NA WALIPOTEZA MAISHA YAO PAPO HAPO NA
MMOJA KUPATA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA
WILAYA YA NYAMAGANA (BUTIMBA).
WALIOUAWA,
1. FERUZ ISMAIL ELIAS MIKA 27, MUHA IMAMU WA MSIKITI HUO NA MKAZI WA
IBANDA RELINI, 2. MBWANA RAJAB MIAKA 40, MBONDEI MFANYABIASHARA NA MKAZI
WA IBANDA, 3. KHAMISI MPONDA MIAKA 28 DEREVA WA KIWANDA CHA SAMAKI
(TFP), MKAZI WA MKOLANI, WOTE WALIJERUHIWA SEHEMU ZA KICHWANI, SHINGONI
NA MIKONONI.
ALIYEJERUHIWA NI ISMAIL ABEID @ GHATI MIAKA 13, MKURYA
MWANAFUNZI WA MADRASA KATIKA SHULE YA KIISLAMU ITWAYO JABAR HILA
ILIYOKO MAENEO YA NYASAKA ALIYEPATA MAJERAHA KICHWANI NA ANAPATA
MATIBABU HOSPITALI YA NYAMAGANA.
KUTOKANA
NA HALI HIYO, WAUMINI WENGINE WALIFANIKIWA KUKIMBIA HUKU WAKIPIGA
MAYOWE YALIYOPELEKEA WAHALIFU HAO KUKIMBIA NA KURUSHA NDANI YA MSIKITI
CHUPA MBILI ZA KONYAGI ZILIZOKUWA NA PETROLI NA TAMBI ZA MOTO, CHUPA
MOJA ILILIPUKA LAKINI HAIKULETA MADHARA MAKUBWA.
JESHILA
LA POLISI LIMEWAKAMATA WASHUKIWA WATATU KWA AJILI YA KUWAHOJI
KUHUSIANA NA TUKIO HILO, HUKU MSAKO MKALI WA KUWASAKA WATU WENGINE WALIO
HUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KWENYE MAUAJI HAYO UKIWA BADO
UNAENDELEA.
NAPENDA KUWAELEZA WANANCHI WATULIE WAKATI TUKIENDELEA NA
UPELELEZI WA TUKIO HILI, NA NATOA WITO KWA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA
JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU WA MAUAJI HAYO ILI TUWEZE
KUWAKAMATA.
PIA NASHAURI NA KUSISITIZA KUWEPO NA KAMATI ZA ULINZI NA
USALAMA KATIKA NYUMBA ZA IBADA, KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA MITAA YAO.
HII ITASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA
MAENEO HAYO.
IMESAINIWA NA:
……………………….
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
No comments:
Post a Comment