Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, May 19, 2016

MADEREVA BODA BODA MJINI NJOMBE WALALAMIKIA KUKATIWA STAKABADHI ZA USHURU WA MAZAO KAMA STIKA ZA MAEGESHO

 
 STAKABADHI HIZO NI HIZI AMBAZO UNAZIONA APA

 




 HAWA NI MADEREVA WA BODABODA WALIPOKUWA  KWENYE KIKAO KIFUPI



 PIA WAMELALAMIKIA KUOMBWA RUSHWA  NA BAADHI YA WAFANYA KAZI WA WAKALA HUYO




STAKABADHI  HIZI HAZINA HATA MIHURI YA KAMPUNI HUSIKA
 HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE IMEPIGA MARUFUKU WANANCHI KUTOA FEDHA  NA KUKATIWA STAKABADHI KAMA HIZI LAKINI YASHANGAZA BADO  ZINAENDELEA KUTOLEWA NA MAWAKALA







HAWA NI MADEREVA WA PIKIPIKI MAARUFU KAMA BODABODA



Wamiliki Na Madereva Wa Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Mjini Njombe Wameitupia Lawama Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Na  Mamlaka Zinazohusika  Na Usimamizi Wa  Tozo  Za Vyombo Vya Moto  Ambazo  Bado Stakabadhi Zake Zinatolewa  Zilizoandikwa Kwa Mkono Licha Ya Halmashauri  Hiyo Kupiga Marufuku  Stakabadhi  Hizo.

Wakizungumza  Kwenye Kikao Kifupi Kilichowakutanisha  Madereva  Wa Pikipiki Katika Uwanja Wa National Housing  Wamesema Licha Ya Halmashauri Hiyo Kutangaza Kwamba  Stakabadhi Zinazotakiwa Kutolewa Na Mamlaka Zote Zinazohusika Na Uchangishaji Wa Fedha  Na Mapato    Ya Halmashauri  Ziwe Za Kwenye Mashine Za Kielectronic  Lakini Bado Wanapewa Zilizoandikwa Kwa Mkono.

Aidha Madereva Hao Wamekosoa Mpango Wa Mawakala Waliowekwa Na Halmashauri Ya Mji Wa Njombe  Wa Kuwapatia Stakabadhi Zilizo Andikwa   Michango Ya Ushuru Wa Mazao Na  Misitu  Ikiwa Wao Hawauzi Mazao Wala Mbao Za Misitu Jambo  Lililosababisha  Kukosa Imani Na Mawakala  Wanaochukua Tozo Za Maegesho   Kuwa Huenda Zikawa Zinaishia Mifukoni Kwa Watu Wachache.

Katika Hatua Nyingine Madereva Hao Wamelilalamikia Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Kwa Kushindwa Kutekeleza Agizo La Mkuu Wa Jeshi La Polisi Wilaya Ya Njombe   OCD Msolo  Hamisi Msolo Alilotoa Siku Ya Kikao Baina Ya Madereva Bajaji,Madereva Daladala Na Madereva Wa Pikipiki,  Agizo Ambalo Lilikemea Tabia Ya Watu Wasiyo Maafisa Usalama Wa Barabarani Kujihusisha Na Ukamataji   Wa Vyombo Vya Moto.

Akizungumza Mbele Ya Madereva Hao  Mwenyekiti Wa Madereva Wa Bodaboda Wilaya Ya Njombe  Filemon Mwinuka Ameunga Mkono  Malalamiko Ya Madereva Hao Kwa Kusema Wamekuwa Wakinyanyasika Na Kuyumbishwa Na Watu Wanaojiita Mawakala  Ambao Wamekuwa Wakikamata Pikipiki  Na Magari Madogo Aina Ya Tax Kwaajili Ya Maegezo Ikiwa Wao Hawana Utalaamu Wowote Wa Kukamata Vyombo Vya  Moto.

Bwana Mwinuka Ametaka Pia Madereva Hao Kufuata Sheria Na Kanuni Za Usalaama Wa Barabarani Kwa Kuacha Kubeba  Abiria  Zaidi Ya  Mmoja,Kuvaa Kofia Ngumu Kila Anapoendesha Pikipiki  Huku Kampeni Ya Kukamata  Baadhi Yao Wanaokiuka Taratibu Zilizoanishwa Na Maafisa Usalama Wa Barabarani Na  Sumatra  ikiendelea Kwaajili Ya Usalaama Wa Mwendeshaji Mwenyewe.

Siku Chache Zilizopita  Ilimunukuu Afisa Habari Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Yasinta  Kisima Akisema  Wananchi Hawatakiwi Kutoa Pesa Ya Aina Yoyote Ile Kwa Watendaji Na Mawakala Watakao Chukua Fedha  Na Kutoa Stakabadhi Zilizoandikwa Kwa Mkono Huku Jeshi La Polisi Nalo Lilitoa Agizo Kwamba Haruhusiwi Mtu Yeyote  Kukamata  Vyombo Vya Moto Ambaye Siyo Afisa Usalama Wa Barabarani Agizo Ambalo Limeonekana Kupuuzwa Na  Baadhi Ya Mawakala.


No comments:

Post a Comment