HAWA NI WAZEE WA KATA YA KIDEGEMBYE NAO WANUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI TASAF SASA WATAKA SERIKALI IFIKILIA MATIBABU BURE KWA WAZEE NA PENSHEN
WAKATI WAKIWA KWENYE ZOEZI LA KUPOKEA FEDHA HIZO
WANUFAIKA HAO WAKISHAPEWA FEDHA HIZO ZINAWANUFAISHA KATIKA SWALA LA MATIBABU NA HAPA NI ZAHANATI AMBAYO IPO KWA MANUFAA YA WAKAZI HAO
MANANASI NAYO NI MIONGOZI MWA KILIMO WANACHOJIKITA KULIMA
MASHAMBA YA MIWA NAYO YAHUSIKA KATIKA KILIMO KWA WANUFAIKA WA MPANGO WA TASAF
Wakizungumza Na Uplands Fm Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Madeke Wamepongeza Mtaalamu Wa Kilimo Kata Na Kijiji Hicho Kwa Kuhamasisha Wananchi Kutumia Kilimo Hai Katika Kilimo Cha Mananasi Na Mazao Mbalimbali Yanayostawi Pasipo Kutumia Mbolea Za Chumvichumvi Ambapo Pamoja Na Kilimo Hicho Lakini Bado Changamoto Ya Soko La Kuuzia Matunda Hayo Ni Changamoto Kwao.
Aidha Wananchi Hao Wamesema Vifaa Vya Mashine Ya Kusindika Mananasi Katika Kijiji Hicho Tangu Ipelekwe Na Halmashauri Ina Takribani Zaidi Ya Miaka Mitatu Mashine Haifanyi Kazi Ikiwa Wakulima Wameongeza Kilimo Cha Manansi Kutoka Kwenye Ekari Moja Hadi Ekari Sita Kwa Mkulima Mmoja Ambapo Changamoto Kubwa Matunda Hayo Yanaozea Mashambani Kwa Kukosa Soko.
Hata Hivyo Wananchi Hao Wamesema Kinachochangia Kwa Kiasi Kikubwa Kukosa Hata Soko La Ndani Ya Mkoa Wa Njombe Na Mkoa Jirani Wa Morogoro Ni Uwepo Wa Miundombinu Mibovu Ya Barabara Ambazo Hazipitiki Kwa Msimu Wa Mvua Na Kusababisha Magari Kikwama Na Kulaza Mizingo Polini Jambo Ambalo Wamiliki Wa Magari Hawataki Kupeleka Magari Yao Huko.
Akizungumza Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Madeke Dikray Kyerula Amekili Kuwepo Kwa Changamoto Ya Wakulima Wa Kilimo Hai Kukabiliwa Na Tatizo La Kukosekana Kwa Soko La Matunda Licha Ya Halmashauri Kuweka Mikakati Ya Kupeleka Mashine Ya Kusindika Matunda Huku Akisema Matunda Mengi Yanaozea Shambani Kwa Kukosa Wateja.
Akizungumzia Kilimo Hai Kinavyoweza Kuwanufaisha Wakulima Wa Matunda Katika Kijiji Cha Madeke Afisa Kilimo Na Mifugo Onesmo Mfugale Amesema Serikali Iko Mbioni Kulitafutia Ufumbuzi Tatizo La Soko Kwa Kukamilisha Miundombinu Ya Kiwanda Cha Kusindika Mananasi Na Matunda Mengine Kama Maparachichi Na Matunda Mengine Huku Akisisitiza Wananchi Kutumia Kilimo Hai Kupata Soko Zaidi.
Kwa Upande Wake Diwani Wa Kata Ya Mfriga Vasco Mgunda Amesema Serikali Inaendelea Na Jitihada Za Kutatua Changamoto Ya Miundombinu Ya Barabara Zinazoelekea Kwenye Kata Hiyo Za Kuwatafuta Wadau Mbalimbali Wa Kununua Matunda Katika Kata Ya Mfriga Ambapo Kuhusu Kiwanda Cha Kusindika Matunda Amesema Bado Hajafuatilia Kujua Tatizo Lake Na Kuahidi Kufatilia Halmashauri Kufahamu Kinachokwamisha Kuanza Kufanya Kazi.
No comments:
Post a Comment