HAPA NDIYO MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Mjini Njombe Leo Imetupilia Mbali Kesi ya Uchaguzi Mkuu Namba 6 ya Mwaka 2015 nafasi ya Ubunge Jimbo la Njombe Mjini Iliyofunguliwa na Aliyekuwa Mgombea Ubunge Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Emmanuel Godfrey Masonga Dhidi ya Edward Mwalongo Aliyetangazwa Mshindi Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.
Kesi Hiyo Iliyovuta Hisia za Watu Wengi Katika Mahakama Hiyo Kwa Takribani Kipindi Cha Miezi Mitano Tangu Ifunguliwe Katika Mahakama Hiyo Imefikia Hatua Hiyo Kutokana na Kifungu Cha Sheria Cha 108 Kidogo B Kinachomtaka Mdai Kuithibitishia Mahakama Juu ya Kesi Yake Bila Kuacha Shaka Yoyote.
Akitoa Hukumu Hiyo Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Jacob Mwambegele Amesema Kwa Mujibu wa Kifungu Cha 108 Kidogo B Kinamtaka Mdai Kuithibitishia Mahakama Bila Kuacha Shaka Yoyote Jambo Ambalo Kipengele Hiki Kimeifanya Mahakama Kushindwa Kuridhishwa na Ushahidi wa Mdai Bwana Masonga Hususani Kipengele Cha Kushindwa Kupeleka Malalamiko ya Tuhuma za Kampeni za Ukabila Kwenye Kamati ya Maadili Ya Jimbo Tangu Kampeni Zinaanza.
Jaji Mwambegele Amesema Mahakama Hiyo Pia Imeshindwa Kuridhishwa na Kitendo Cha Mdai Huyo Kufanikiwa Kupeleka Mapingamizi Ambayo Hayakuwa na Msingi Mkubwa Kama la Ukabila Jambo Ambalo Mahakama Inaamini Kesi Hiyo Imefunguliwa Baada ya Kushindwa Katika Uchaguzi Huo Yaani[AFTER THOUGHT] na Kuacha Shaka Katika Ushahidi Wake.
Nje ya Mahakama Uplands Fm Imezungumza na Wakili wa Mdai Edwin Swale Ambaye Amesema Hajaridhishwa na Uamuzi wa Mahakama Hiyo Huku Emmanuel Masonga Akisema Anakwenda Kukaa na Chama Chake Cha CHADEMA na Atatoa Taarifa Kwa Wananchi.
Samson Rutebuka ni Wakili wa Mbunge Edward Mwalongo wa CCM Ambaye Amesema Ameridhishwa na Hukumu Iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Hiyo Huku Mbunge Esdward Mwalongo Akisema Amefanikiwa Kushindwa Mara Mbili Kwa Boxi na Mahakamani na Hivyo Kinachotakiwa ni Kuwatumikia Wana jimbo la Njombe Mjini Wote.
No comments:
Post a Comment