Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, March 21, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO AONGOZA KUAGA MWILI WA MAREHEM MWANJISI

Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(mwenye miwani) akiwa amebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu mkuu wa zamani Wizara ya Habari Marehemu Frank P. Mwanjisi aliyefariki jijini Dar es Salaam.Marehemu amesafirishwa leo kwenda mbeya kwa ajili ya mazishi.
Mchungaji kutoka kanisa la KKKT usharika wa kariakoo akiendesha misa ya kumuombea marehemu Frank Mwanjisi ambaye aliwahi kushika wadhifa wa katibu mkuu katika wizara ya Habari. Picha na Daudi Manongi-WHUSM.
Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akimpa pole Elifasi Mwanjisi ambaye ni mdogo wa marehemu Frank Mwanjisi aliyekuwa katibu mkuu wa zamani Wizara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa katibu mkuu wa zamani wa wizara ya Habari Marehemu Frank Mwanjisi aliyefariki jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa marehemu ,Bw Charles Mwanjisi(mwenye t-shirt nyeusi) akizungumza jambo na mkurugenzi msaidizi-MAELEZO Bw.Raphael Hokororo wakati wa misa.

No comments:

Post a Comment