
Na Woinde Shizza,Simanjiro
Mpango
mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la awali mpaka sekondari umeonekana
kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno hususani
jamii ya kifugaji kutoka katika kijiji cha Kichangare wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua kumkodisha mwalimu na
kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.
Wanafunzi
wa shule hii ya msingi Kichagare wamekuwa wanajisomea wakiwa wamekaa
chini huku shule hiyo ikiwa imeezekwa na vipande vya turubai ili kuweza
kupata ahueni wakati wakujisomea ambapolengo la wazazi wao kufanya
hivyo ni kuwasaidia watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na
karne hii ya sasa ya teknolojia.
Gazeti
hili lilibahatika kufika eneo la tukio na kuzungumza na mwalimu wa shule
hiyoaliyejitambulisha kwa jina la Lilian Nanyaro ambapo alisema kuwa
aliamuakujitolea kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare
kitongoji cha Loongung hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia
wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .
Alisema
kuwa mazingira ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika
swala zima la ufundishaji kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo
ukizingatia kwamba watoto ambao ni wanafunzi wana nia ya kutaka
kusoma.
‘’ndugu
mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu hamna paa
paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka na pia
ukiangalia mazingira ya kijiji chetu mvua zinaponyesha pia inakuwa ni
tatizo kubwa sana kwani inafikia mahali wanafunzi hushindwa kufika
shule kabisa nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza
kutusaidia tatizo hili kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya
kusomea itawasadia sana hivo wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema
Nanyaro.
Kwa
upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina
la Seigulu James alisema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma
lakini tatizo kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana
,kwani kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.
Alitumia
fursa hiyo kuiomba serekali kuwasaidia kuweza kupata angalau madawati
pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na kuwapatia walimu
ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama wanafunzi
wengine na watoto wa shule zingine.
Honie
Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro alisema kuwa
wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu mmoja ambaye ndio
wanae hapo shule ambapo alisema wao kama wanakijiji wanajichangisha ela
na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.
“sisi
tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute mwalimu ambaye
atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo tunajichanga
tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia shilingi
elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye
Kwa
upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet Losijake alisema
kuwa mapaka sasa tayari vikao vyao vya bajeti halmashauri wameshaomba
kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu wa
darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.
Wahenga
wanamsemo usemao usipoziba ufa utajenga ukuta,hivyo ni vyema kama
serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu kuangalia eneo hilo kwa
ukaribu ili kuweza kuwaondolea changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi n
ahata mwalimu kufundisha katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment