Tuesday, January 12, 2016
WANANCHI WATAKIWA KUFUGA NYUKI NA KUPANDA MITI YA MATUNDA AINA YA PARACHICHI
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FORE STERING ECONOMIC ATUKUZWE MWENDAMSEKE
Shirika La Fore Stering Economy Linalojihusisha Na Utunzaji Wa Mazingira Mkoani Njombe Limewataka Wananchi Kutunza Mazingira Kwa Kupanda Miti Yenye Maua Kwaajili Ya Chakula Cha Wadudu Wa Porini Hususani Nyuki Pamoja Na Wananchi Hao Kuhusika Na Utengenezaji Wa Mizinga Kwaajili Ya Kufunga Nyuki.
Akizungumza Na Mtandao Huu Mkurugenzi Wa Shirika Hilo Atukuzwe Mwendamseke Amesema Shirika La Fore Stering Economy Pia Linatoa Elimu Ya Ujasiliamali Na Elimu Ya Kujitegemea Kwa Kujiajiri Kwa Baadhi Ya Vijana Ambao Wanatoka Vyuoni Na Shuleni Na Kusaidia Kuondoa Utegemezi Wa Kupatiwa Ajira Serikalini Badala Yake Wajiajiri.
Aidha Mwendamseke Amesema Shirika Hilo Limejipanga Kutoa Elimu Ya Uhifadhi Na Namna Ya Kulina Asali Kwa Njia Ya Kisasa Kwa Wafugaji Wa Nyuki Ili Wapate Soko La Asali Nchini Na Nje Ya Nchi Ambapo Amesema Kwa Anayehitaji Kufuga Wadudu Hao Anapaswa Kupanda Hata Miti Ya Miparachichi Ambayo Itawapatia Faida Mara Dufu.
Mwendamseke Amepongeza Wananchi Wa Wilaya Ya Ludewa Kwa Kuongeza Jitihada Za Kufuga Nyuki Licha Yakuwepo Kwa Changamoto Ndogo Ya Kuhifadhi Asali Na Nnta Na Kwamba Kuna Kampuni Ya Manongo Imeanza Kukusanya Asali Na Nnta Zinazopatikana Kwa Wafugaji Wa Nyuki Mkoani Njombe.
Kwa Upande Wake Baadhi Ya Wafugaji Wa Kutoka Lupembe Na Baadhi Ya Maeneo Ya Ludewa Wameomba Elimu Kutolewa Kwa Wingi Kwa Wafugaji Hao Wa Nyuki Kwa Kushirikiana Na Serikali Ili Kufanikisha Zoezi La Ufugaji Huo Kuliko Kuliachia Shirika Peke Yake Kutoa Elimu Hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment