Tuesday, January 12, 2016
VYOMBO VYA MOTO VYA TAKIWA KUFUATA SHERIA ,KANUNI NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
AFISA USALAMA WA BARABARANI HAPPY ROSE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI AKIWA KATIKA OFISI ZA UPLANDS RADIO NJOMBE
MKAGUZI WA MAGARI NMKOA WA NJOMBE COPLO WILLIAM KATIKA PICHA
Jeshi La Polisi Mkoani Njombe Limewataka Watumiaji Wa Vyombo Vya Moto Kufuata Kanuni Na Sheria Za Usalama Barabarani Ili Kuepusha Ajali Na Kwamba Jeshi La Polisi Limejipanga Kukomesha Tabia Za Kuendesha Vyombo Vya Moto Kwa Kasi .
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Afisa Usalama Barabarani Happy Rose Amesema Jeshi La Polisi Limekuwa Likitoa Elimu Ya Usalaama Barabarani Kupitia Vyombo Vya Habari Vya Mkoa Wa Njombe Pamoja Na Kuwakumbusha Madereva Juu Ya Alama za Usalama Barabarani Ili Kupunguza Ajari Hizo.
Aidha Rose Amesema Chanzo Kikubwa Cha Ajali Hizo Kinatokana na Baadhi ya Madereva Wengi Kutumia Vibaya Vyombo Vyao Vya Moto Na Kwamba Jeshi la Polisi Linasimamia Sheria Kwa Madereva Wanaokiuka Sheria Hizo Ambapo Hatua Mbalimbali Zimekuwa Zikichukuliwa Dhidi Ya Wanaokiuka Kwa Kuwaelimisha Na Kutaka Waheshimu Alama Hizo.
Kwa Upande Wake Mkaguzi Wa Magari Mkoa Wa Njombe Coplo William Amesema Suala La Mwendo Kasi Barabarani Linatakiwa Kuheshimiwa Na Madereva Wote Wa Vyombo Vya Moto Wakiwemo Waendesha Pikipiki Na Magari Na Kutumia Elimu Walizozipata Wakiwa Darasani Kuzitumia Na Kuzitambua Na Kutafsiri Alama Hizo Kuepusha Ajali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment