DIWANI WA KATA YA ITULAHUMBA TITO MDENDEMI AZUIA MZEE MGUTE ASIUZE NYUMBA YA WATOTO WAO KATIKA KIJIJI CHA ISINDAGOSI
DIWANI WA KATA YA ITULAHUMBA BAADA YA KUWASILI KWENYE NYUMBA WANAYOISHI WATOTO WA MZEE MGUTE AMBAYE ANALALAMIKIWA KUTAKA KUUZA NYUMBA NA MAENEO HUKU WATOTO WAKIWA NDANI NA MAMA YAO ALIKWISHA KUFARIKI SASA WATOTO WANASEMA WAENDE WAPI.
WATOTO AMBAO MAMA YAO ALIKWISHA FARIKI PENDO MGUTE ,WAKIWA NA KAKA YAO WENGINE HAPA HAWAPO KWA MAMA ALIYE FARIKI WAKO WANNE WOTE WAKIKE LAKINI HUYU KAKA YAO NI WA MAMA MWINGINE LAKINI WALIKUWA MTU NA DADA WALIOLEWA KWA MTU MMOJA HIVYO KAKA HUYU ANAWASAIDIA DADA ZAKE WASIONDOLEWA KWENYE NYUMBA YA MAREHEMU MAMA YAO
HAWA NI BAADHI TU YA WANANCHI WALIOKOMALIA JAMBO HILO HADI HAPO LILIPOFIKIA KUHAKIKISHA MWENYEKITI NA MZEE MGUTE HAWAUZI NYUMBA HIZO ZA WATOTO
DIWANI MDENDEMI AKIWA NA WANANCHI PAMOJA NA WATOTO WA MZEE MGUTE
ENEO LENYEWE WANALOTAKA KUUZA NI HILI LA NYUMBA YA WATOTO HAO
HUYU NDIYE DIWANI WA KATA YA ITULAHUMBA WILAYANI WANGING'OMBE TITO MDENDEMI
DIWANI WA KATA YA ITULAHUMBA TITO MDENDEMI AKIHOJIANO JUU YA WATOTO WALIOUZIWA NYUMBA NA MAENEO NA BABA YAO
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA ISINDAGOSI ZEBEDAYO DEGE AKITOLEA UFAFANUZI JUU YA TUHUMA ZINAZOMKABILI YEYE NA MZEE MGUTE AKIWA OFISINI KWAKE
Diwani Wa Kata Ya Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Tito Mdendemi Ameagiza Kusimamishwa Kwa Zoezi La Kuuzwa Kwa Nyumba Ya Watoto Wa Mzee Meck Mgute Ambaye Ametuhumiwa Kutaka Kuuza Nyumba Na Maeneo Ya Watoto Wake Wanne Ambao Hawana Mama Yao Wanaoishi Katika Kijiji Cha Isindagosi.
Agizo Hilo Amelitoa Diwani Wa Kata Hiyo Mdendemi Baada Ya Kusikiliza Malalamiko Ya Majirani Na Watoto Wa Mzee Mgute Ambaye Ni Baba Wa Watoto Hao Akishilikiana Na Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Isindagosi Kwamba Wameuza Nyumba Na Maeneo Wanayoishi Watoto Wa Mzee Huyo Na Kuwafukuza Wakaishi Wanakojua Wao.
Mdendemi Amesema Wakati Akifuatilia Kwenye Baraza La Kata Kujiridhisha Kama Watoto Hao Wamefungua Kesi Ya Kuuzwa Nyumba Na Eneo La Marehemu Mama Yao Ikiwa Wao Bado Wanaishi Kwenye Nyumba Hiyo Wananchi Wa Kijiji Cha Isindagosi Wanapaswa Kumpatia Taarifa Mara Moja Endapo Kuna Watu Wamefika Kuwahamisha Watoto Hao Ili Sheria Ifuate Mkondo Wake.
Wakizungumza Mbele Ya Diwani Wa Kata Ya Itulahumba Tito Mdendemi,Watoto Wa Mzee Meck Mgute Wakiongozwa Dada Yao Mkubwa Pendo Mgute Akishilikiana Na Kaka Yao Ambaye Ni Mtoto Wa Mama Mdogo Wa Familia Hiyo Ben Mgute Wamemueleza Diwani Huyo Kwamba Mwenyekiti Na Baba Yao Meck Mgute Wameshilikiana Kuwafukuza Watoto Kwenye Nyumba Ya Marehemu Mama Yao Kwa Kuuza Kwa Shilingi Laki Nane.
Mtandao Huu Umeongozana Na Diwani Wa Kata Hiyo Tito Mdendemi Na Kukutana Na Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Isindagosi Ambaye Analalamikiwa Kushilikiana Na Mzee Mgute Kuwahamisha Watoto Hao Zebedayo Dege Amekanusha Kuhusika Na Tuhuma Hizo Huku Akikili Kupokea Taarifa Za Kuuzwa Kwa Eneo Hilo Toka Kwa Mzee Mgute.
Awali Wananchi Wa Kijiji Cha Isindagosi Kata Ya Itulahumba Wakizungumza Na Uplands Fm Wameutupia Lawama Uongozi Wa Kijiji Hicho Hususani Mwenyekiti Kwa Kuhusika Kutumia Madaraka Yake Vibaya Kuwashawishi Baadhi Ya Wananchi Wauze Maeneo Yao Ili Pesa Wampatiye Na Yeye Ikiwemo Kusimamia Kuuzwa Kwa Eneo La Familia Ya Watoto Wanne Licha Ya Mwenyekiti Huyo Kukanusha Malalamiko Hayo.
No comments:
Post a Comment